
Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, imewahukumu kifungo cha maisha jela Suleiman Thabit Ngulangwa na Farid Hamis Said baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la biashara haramu ya dawa za kulevya aina ya heroin yenye uzito wa kilo 15.19.
Katika hukumu iliyotolewa Juni 1, 2026, Jaji S.E. Kisanya alisema ushahidi wa upande wa mashtaka ulithibitisha pasipo shaka kuwa washtakiwa hao walikuwa na umiliki wa dawa hizo.
Mchambuzi wa Serikali kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Leonida Daniel Michael, aliithibitishia mahakama kuwa pakiti 16 zilizokamatwa zilikuwa na heroin yenye uzito wa kilo 15.19 baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kisayansi.
Mahakama ilibaini kuwa utetezi wa washtakiwa haukuweza kuibua shaka dhidi ya ushahidi wa mashahidi na vielelezo vilivyowasilishwa.
Mshtakiwa wa pili, Sharifa Selemani Bakari, aliachiliwa huru baada ya mahakama kubaini kuwa upande wa mashtaka haukuthibitisha ushiriki wake katika kosa hilo.
Mbali na kifungo hicho, mahakama imeagiza heroin yote iliyokamatwa pamoja na vifaa vya kufungashia kuteketezwa kwa mujibu wa sheria.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment