Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ruvuma limefanya ziara ya kiutendaji katika Kitongoji cha Kisendema, Kata ya Msisima, Wilaya ya Namtumbo, kwa lengo la kutoa elimu kuhusu umuhimu wa utunzaji wa miundombinu ya umeme. Ziara hiyo pia ilitoa fursa kwa wananchi kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili katika upatikanaji wa huduma za umeme na kupata ufafanuzi wa masuala yanayohusu huduma za TANESCO.Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma, Bw. Allan Njiro, alisema kuwa lengo la kuwafikia wananchi katika maeneo yao ni kujenga uelewa wa pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya TANESCO na jamii. Alisisitiza umuhimu wa wananchi kutoa taarifa za changamoto kwa wakati ili ziweze kushughulikiwa mapema na kwa ufanisi.Bw. Njiro pia aliwahimiza wananchi kutunza miundombinu ya umeme kwa kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha uharibifu wake. Alitaja baadhi ya vitendo hivyo kuwa ni uchomaji moto ovyo karibu na miundombinu ya umeme pamoja na ukataji miti holela unaoweza kuhatarisha usalama wa nguzo na nyaya za umeme.Kwa upande wao wananchi wameonesha kufurahishwa na hatua ya TANESCO kufika moja kwa moja katika eneo lao kusikiliza na kutatua changamoto zao. Walisema mikutano ya aina hiyo inasaidia kuongeza uelewa kuhusu huduma za umeme, kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi na taasisi za umma, pamoja na kujenga imani inayochochea maendeleo ya jamii.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment