Wafanyabiashara na wamiliki wa vibanda katika Stendi ya Mabasi, Kata ya Murusi, Halmashauri ya Mji Kasulu wametakiwa kuwa mabalozi wa utunzaji wa mazingira kwa kuhakikisha wanafanya usafi wa maeneo yao ya biashara mara kwa mara na kumiliki vifaa vya kuhifadhia taka (dustbin).Maelekezo hayo yametolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Anthony Mwakisu wakati anazungumza na wafanyabiashara wa stendi hiyo, akiwasisitiza kununua na kuweka dustbin kubwa mbele ya maeneo yao ya kazi ili kutunza taka zote humo na kuahidi kuwa atafanya ukaguzi binafsi kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa.Katika hatua nyingine, Kanali Mwakisu amewaagiza kukatia na kumwagilia maua yote yaliyo ndani ya Stendi sambamba na kufanya kazi kwa ushirikiano, uadilifu na utii ili kuboresha mazingira na kuifanya stendi kuwa safi na yenye kuvutia.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia Julius Simbeye, amesema ushiriki wa viongozi katika zoezi la usafi unalenga kuhamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kufanya usafi kila siku katika maeneo yao ya biashara na makazi, huku akisisitiza kuzingatia taratibu za usafi wa mazingira ili kuifanya Kasulu kuwa mji safi na wenye afya bora.Mratibu wa shuughuli za usafi na udhibiti wa taka Halmashauri ya Mji Kasulu, Msafiri Nimbili Charles amewahimiza wananchi kuzingatia usafi wa mazingira, lishe bora na kufanya mazoezi ili kujenga jamii yenye afya. Zoezi hilo la usafi limefanyika kwa ushirikiano mkubwa kati ya viongozi, wananchi, wafanyabiashara, Kasuku na Mwandiga Jogging Club.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

















Post a Comment