
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tabora, Cde. Rashid Ramadhan, maarufu kama Kamanda Tall, enzi za uhai wake.
Tabora.
DIWANI wa Kata ya Chemchem wilaya ya Tabora, Bandora Salum Mirambo, ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tabora, Cde. Rashid Ramadhan, maarufu kama Kamanda Tall, aliyefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Kitete.
Akitoa salamu hizo, Bandora amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha kiongozi huyo, akieleza kuwa marehemu alikuwa mshauri wake wa karibu na kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika kuimarisha na kujenga Chama Cha Mapinduzi ndani ya Wilaya ya Tabora na Mkoa kwa ujumla.
"Nimesikitishwa sana na kifo hiki. Marehemu alikuwa mtu muhimu sana kwangu, aliyekuwa akinishauri na kuniongoza katika majukumu mbalimbali, pia alikuwa na mchango mkubwa katika ujenzi na maendeleo ya Chama Cha Mapinduzi katika wilaya na mkoa kwa ujumla," amesema Bandora.
Ameongeza kuwa enzi za uhai wake, marehemu alijitolea kusimamia haki, kuzingatia misingi ya chama, pamoja na kudumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama na wananchi.
Bandora ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki, wanachama wa CCM na wananchi wote walioguswa na msiba huo, huku akiwaombea uvumilivu na nguvu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
"Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina."
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment