Halmashauri ya Mji imepongezwa kwa kupata Hati Safi ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2025 ikiwa ni matokeo ya ukaguzi uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).Pongezi hizo zimetolewa na Mgeni Rasmi, Balozi Simon Sirro wakati akizungumza katika kikao cha kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kilichofanyika katika Ukumbi wa Fatina H. Laay wa Halmashauri ya Mji. Balozi Sirro amewapongeza viongozi na watumishi wa Halmashauri kwa kazi wanazoendelea kufanya ambapo ameelekeza kuimarisha suala la ulinzi na usalama, kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani pamoja na kuhakikisha matumizi sahihi ya fedha za umma.Kwa upande wake, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Kigoma amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi, inakamilika kwa wakati na kuendelea kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi.Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Katibu Tawala wa Wilaya Bi. Theresia Mtewele ameahidi kuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya itaendelea kushirikiana kwa karibu na Halmashauri katika kuhakikisha mapendekezo yote ya ukaguzi yanatekelezwa ipasavyo na kuwataka wakuu wa idara na watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano, uwajibikaji na weledi.Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mhe. Ayubu Ngalaba Kilugu pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mwl. Vumilia Julius Simbeye, wamsahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa ili kuchochea maendeleo na ustawi wa wananchi.Awali, Madiwani walipata fursa ya kusikiliza taarifa na kuunga mkono hoja na mapendekezo yaliyowasilishwa pamoja na kuahidi kushirikiana kikamilifu katika utekelezaji majukumu yao kwa lengo la kuendelea kuimarisha utendaji wao wa kazi.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254














Post a Comment