" Katambi atema nyongo

Katambi atema nyongo

Na Mwandishi Maalumu

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema hatakuwa tayari kuona kundi la watu wenye maslahi binafsi likichezea amani ya nchi na kusisitiza yupo tayari kwenda mahakamani hata usiku ili jamii ipate suluhu ya wapotoshaji wanaotumika kuchochea chuki na kuhatarisha usalama. 

Alitoa msimamo huo kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza na makundi ya walinzi wa amani katika jamii, polisi jamii, wazee, sungusungu, wenyeviti wa mitaa, mabalozi, na wenyeviti wa vitongoji mjini Shinyanga, akieleza kuwa bado hajapokea wito wa kuitwa mahakamani lakini atakwenda bila kusita endapo utafika hata kama ni usiku wa manane. 

Alisema mahakama ni chombo huru chenye mamlaka ya kusema Katiba imevunjwa na si jukumu la mtu au taasisi binafsi kujichukulia mamlaka hayo yasiyo sahihi, akibainisha kuwa timu inayotishia kumpeleka mahakamani ndiyo hiyo hiyo iliyokuwa ikipinga mkataba wa uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam ambayo kwa sasa inaingiza fedha nyingi kwa taifa. Waziri huyo alihoji ukimya wa watu hao dhidi ya matendo ya hatarishi ya uchochezi yanayolenga kuangamiza nchi kupitia uchomaji wa shule, vituo vya mafuta, ofisi za serikali, mali na biashara za watu binafsi, pamoja na uvamizi wa vituo vya polisi, akisisitiza kuwa hawajawahi kukemea vitendo hivyo vinavyotishia uhai wa wananchi.

Alibainisha kuwa wamepewa dhamana ya kulinda amani ya nchi kwa viapo vyao na watailinda kwa gharama zote ili kuzuia madhara kama vile kupoteza mvuto kwa watalii, kuwekewa vikwazo kwa nchi, kusimama kwa miradi mikubwa ya maendeleo, kubomoka kwa mahusiano ya kidiplomasia, na kutisha wawekezaji ambao huchangia mapato ya taifa kupitia bandari na sekta nyinginezo. 

Katambi aliwakumbusha Watanzania kuwa hawana nchi nyingine zaidi ya Tanzania huku akitoa mfano wa namna nchi ilivyowahi kuhifadhi wakimbizi kutoka Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) baada ya kukumbwa na machafuko, akionya kuwa wachochezi hao wanapanga fujo wakati familia zao zikiwa nje ya nchi na wakitembea na hati za kusafiria mifukoni, jambo ambalo lingewaacha wazee, watoto, wanawake na wenye ulemavu bila makazi salama endapo amani ingetoweka.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post