KIPATO SHOW, kipindi kipya cha Misalaba Media kinacholenga kuhamasisha wananchi hasa vijana kujishughulisha na shughuli za kujiongezea kipato, kimeanza rasmi kwa mahojiano na Idrisa Rashidi Maganga.
Katika kipindi hicho, Idrisa ameeleza safari yake ya ujasiriamali kupitia kibanda chake kinachotoa huduma mbalimbali za vyakula, ikiwemo chipsi, mishikaki, mihogo, ndizi na kuku, akifafanua namna shughuli hiyo ilivyomwezesha kujipatia kipato na kukidhi mahitaji ya maisha.
Kupitia KIPATO SHOW, watazamaji watapata fursa ya kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali wanaojituma katika kazi na biashara halali, kwa lengo la kuhamasisha jamii kutumia fursa zilizopo na kujenga uchumi wao kupitia bidii na ubunifu.
KIPATO SHOW hurushwa kupitia kurasa zote za mitandao ya kijamii za Misalaba Media.
Wasiliana na Misalaba Media - 0745594231

Post a Comment