*Ukusanyaji mapato ya ndani wapaa kufikia Billions 45.8*Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha.Miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa Jijini Arusha yadhihirisha kasi ya maendeleo kwa siku za usoni na kumvutia Waziri wa Kilimo Daniel Chongolo.Akihutubia Wananchi Jijini humo baada ya kukamilisha ziara yake ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo stendi ya mabasi, nyumba za walimu, uwanja wa AFCON na soko la Kilombero, amesema serikali imewekeza fedha nyingi Ili kuhakikisha Jiji linavutia Watalii na kuingiza fedha nyingi kwa kila mtu.Aidha Kwa kushirikiana na wataalamu wa kilimo amewahakikishia wakulima kwamba serikali italeta pembejeo, mbegu na kufufua zao la Pareto, kuotesha mikorosho katika mabonde na kuweka mifumo ya kilimo cha umwagiliaji."Nawapongeza Halmashauri Kwa kutekeleza miradi mingi Kwa fedha za ndani, hii ni ushuhuda kuwa mnafanya kazi nzuri, nawasihi endeleeni kuhubiri amani Ili serikili sikivu ya awamu ya sita isogeze maendeleo kila mahali"amesema Chongolo.Katika namna hiyohiyo Mkuu wa Wilaya Arusha Joseph MKude amesema Kwa mwaka wa fedha 2025/2026 mapato yaliyokusanywa ni Billions 45.8 sawa na 92% huku serikali kuu (TRA) ikikusanya milions 520.5 sawa na 103.09%.Amesema Bilions 3.4 tayari zimegawiwa Kwa vikundi 272 wanawake, vijana na watu wenye ulemavu."Tunaendelea kutekeleza miradi ya barabara za ndani kwa kwa kasi Chini ya TARURA na TANROADS lengo ni kuwa na miundombinu bora kuelekea mashindano ya AFCON 2027"Vile vile Naibu Meya Julius Ole Sekeyan ameibua kilimo chake mbele ya Waziri Chongolo akiomba serikali kurejesha kilimo cha zao la Pareto Ili iwe mbadala wa wananchi kuachana na kilimo cha Bangi.Amesema Jiji la Arusha lina maeneo mengi ya kilimo ikiwemo mabonde ambayo yakioteshwa korosho itakuwa mlango mpya wa ajira na uchumi Kwa vijana. Hata hivyo ameomba kuwekwa mkakati wa kuvuna maji ya mito kitaalamu Ili yatumike kwenye kilimo badala ya kupotea tu.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment