Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe amepongeza jitihada zinazpendelea kufanywa na Maafisa Afya na Wadau wengine wa afya kuhakikisha takwimu na visa vya milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu zinapungua. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa tathmini ya utekelezaji wa shughuli za afya na usafi wa mazingira Kwa ngazi ya mikoa na halmashauri Tanzania Bara uliofanyika Jijini Arusha, amesema licha ya mapambano ya kupunguza visa vya milipuko ya ugonjwa wa Kipindupindu, amewataka maafisa wa afya kila mkoa kuhakikisha hakuna tena ugonjwa huo nchini ifikapo mwakani.Aidha katika jitihada hizo serikali imepitisha bajeti Kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Billions 35.2, kuhakikisha miundombinu ya shule 274 na Vituo vya afya 274 inakamilika."Natoa wito Kwa shirika la Viwango Tanzania (TBS) kusimamia kikamilifu usalama wa vyakula na vipodozi Ili kulinda afya za walaji, pia kuhakikisha fedha zilizotengwa zinafanya majukumu yake kama ilivyoelekezwa na serikali kuu" amesema Prof.Shemdoe.Katika hatua nyingine Mwakilishi wa UNICEF Religious Sungu amesema wataendelea kushirikiana na serikali katika kampeni ya usafi wa mazingira ikijumuishwa na maboresho ya miundombinu ya afya, Elimu na maji.Vilevile ameeleza kuwa mikoa ya Nyanda za juu kusini ikiwemo Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe imeendelea kufanya vizuri katika suala la usafi wa mazingira, hatua inayoakisi mapambano dhidi ya magonjwa ya milipuko.Hata hivyo akisoma maazimio mbele ya mgeni rasmi Mratibu wa huduma za afya na usafi wa mazingira TAMISEMI Selemani Yondu ameelezea maazimio waliyojiwekea kufikia mafanikio kuwa ni pamoja na ujenzi wa vyoo bora na usafi wa mazingira katika vijiji na kaya, kuendelea kutoa elimu ya matumizi ya miundo mbinu Bora ya vyoo na unawaji mikono na kuanzisha vikundi 1400 vya uhamasishaji elimu hiyo katika jamii.Pia ameiomba ofisi ya Waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kuharakisha fedha za utekelezaji ili kufikia malengo yaliyowekwa."Maazimio mengine tuliyojiwekea ni mamlaka zinazosimamia ubora wa vyakula na vipodozi kwa kila halmashauri kuzingatia na kufanikisha azimio hiilo Ili kulinda afya za walaji ambao ni wananchi" amesema Yondu

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment