Na .Mwandishi wetuDar es salaamDar es Salaam, Julai 23, 2026, Taasisi ya Media Institute of Southern Africa (MISA) Tanzania imepokea vifaa vya kisasa vya kuimarisha usalama wa kidijitali na uwezo wa utendaji wa taasisi kutoka Shirika la DefendDefenders la Uganda, katika hatua inayolenga kuimarisha ulinzi wa taarifa na mifumo ya kidijitali ya taasisi hiyo.Makabidhiano ya vifaa hivyo yalifanyika leo katika Ofisi za MISA Tanzania jijini Dar es Salaam, ambapo mwakilishi wa DefendDefenders, Bw. John Kaoneka, alivikabidhi kwa viongozi wa MISA Tanzania wakiongozwa na Mwenyekiti Edwin Soko. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Makamu Mwenyekiti Rhoda Maruma pamoja na Afisa Utawala Glory Kalinga.Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na kompyuta mpakato (laptop), kamera za ulinzi (CCTV), simu ya mkononi, router, kifaa cha kuhifadhi taarifa (External Hard Drive), Seagate Backup Drive, mfumo wa ulinzi wa kompyuta wa ESET Smart Security pamoja na Wi-Fi SIM Card Router.Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, uongozi wa MISA Tanzania ulieleza kuwa vifaa hivyo vitachangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha usalama wa taarifa za taasisi, kulinda mifumo ya kidijitali, kuboresha mawasiliano na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za kutetea uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza na usalama wa wanahabari nchini.MISA Tanzania imeeleza shukrani zake za dhati kwa DefendDefenders kwa ushirikiano wake wa muda mrefu na msaada huo muhimu, ikibainisha kuwa unadhihirisha dhamira ya pamoja ya kuimarisha taasisi zinazotetea haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na mazingira salama ya utendaji kwa wanahabari.Taasisi hiyo imewahakikishia wanachama wake kuwa vifaa hivyo vitatumika kwa uwazi, uwajibikaji na kwa manufaa ya taasisi na wanachama wake, huku vikichangia kuongeza uwezo wa MISA Tanzania katika kutoa huduma bora na kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment