Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limeendelea kuonyesha dhamira yake ya kushiriki katika shughuli za maendeleo ya jamii baada ya kufanya zoezi la usafi wa mazingira na kuchangia damu salama katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.Zoezi hilo limeusisha maafisa, wakaguzi pamoja na askari wa vyeo mbalimbali, ambao kwa pamoja walifanya usafi katika maeneo tofauti ya hospitali hiyo kwa lengo la kuboresha mazingira ya utoaji huduma za afya. Baada ya shughuli za usafi, askari hao walishiriki kwa hiari kuchangia damu salama ili kusaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo muhimu.Akizungumza baada ta zoezi hilo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Fraterine Tesha amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kutekeleza wajibu wake si tu katika kulinda usalama wa raia na mali zao, bali pia kushiriki shughuli za kijamii zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Aidha, ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga kwa ushirikiano uliowezesha kufanikisha shughuli hiyo.Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga, akizungumza kwa niaba ya uongozi wa hospitali hiyo, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa moyo wa kujitolea na kuthamini umuhimu wa kuchangia damu salama pamoja na kushiriki katika kuboresha mazingira ya hospitali. Ameeleza kuwa mchango huo una thamani kubwa katika kuimarisha huduma za afya na kuokoa maisha ya wagonjwa, huku akiukaribisha tena ushiriki wa Jeshi hilo katika shughuli kama hizo siku zijazo.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254











Post a Comment