" KAMPUNI YA JAMBO GROUP OF COMPANY IMEINGIA MKATABA MPYA WA KUIDHAMINI TIMU YA DODOMA JIJI FC KUELEKEA MSIMU MPYA WA 2026-2027.

KAMPUNI YA JAMBO GROUP OF COMPANY IMEINGIA MKATABA MPYA WA KUIDHAMINI TIMU YA DODOMA JIJI FC KUELEKEA MSIMU MPYA WA 2026-2027.

 

NA EDINGTON EZRON ,MISALABA MEDIA
Uongozi wa timu ya Dodoma jiji football club umefikia makubaliano ya kiuwekezaji na kampuni ya JAMBO GROUP OF COMPANY na kukubaliana kusaini mkataba wa mwaka mmoja ili kuweza kuiwezesha timu hiyo katika uendeshaji.

Mkataba huo umesaidiwa na viongozi wa timu hiyo kwenye ofisi za jambo group zilizopo Manispaa ya Shinyanga katika mkutano wa waandishi wa habari .

Akizungumza katika mkutano huo mtendaji mkuu wa timu ya Dodoma jiji fc Albert Erasto amesema kuwa kupitia udhamini wa kampuni ya jambo msimu uliopita walifanikiwa kwa kiasi kikubwa ikiwemo kujihakikishia kubaki katika ligi ya NBC premier league,kuwa timu pekee iliyofanikiwa kuchukua pointi tatu kwa bingwa wa ligi pamoja na kutoa sare na Simba SC katika uwanja wa nyumbani.

Aidha viongozi hao wamesema kuwa uwekezaji huo umesaidia katika shughuli za mazoezi hasa katika huduma ya maji na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa katika kampuni hiyo.

Hata hivyo viongozi hao wamesema kuelekea msimu ujao wanategemea kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali kwani wamepata fedha ya kutosha kufanya usajili wa wachezaji wenye uzoefu na uwezo wa kiushindani amapo wanategemea kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao.






Post a Comment

Previous Post Next Post