" Mlipuko wa Baruti Waua Mmoja, Wajeruhi Saba Mwanza

Mlipuko wa Baruti Waua Mmoja, Wajeruhi Saba Mwanza


Na Sheila Katikula, MwanzaMtu mmoja amefariki dunia huku watu saba wakijeruhiwa kufuatia mlipuko wa baruti uliotokea katika kibanda cha kahawa kilichopo Mtaa wa Sahwa ya Juu, Kata ya Lwanhima, Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.Tukio hilo lilitokea Julai 1, 2026, majira ya saa 12:46 asubuhi, na kuzua taharuki kubwa miongoni mwa wakazi wa eneo hilo baada ya mlipuko huo kusikika kwa nguvu.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, amesema aliyepoteza maisha ni Marco Msenyere (52), mpasua mawe na mkazi wa Semba-Lwanhima. Kwa mujibu wa Kamanda, marehemu alikuwa amefika katika kibanda hicho akiwa na begi dogo lililokuwa na baruti, huku akiwa ameketi na wenzake wakinywa kahawa.Kamanda Mutafungwa amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha mlipuko huo ni uzembe wa utunzaji wa baruti, baada ya marehemu kukaa na vilipuzi hivyo karibu na jiko la mkaa lililokuwa linawaka, hali iliyosababisha baruti hizo kulipuka kutokana na joto.Waliopata majeraha katika tukio hilo ni Daudi Joseph Baraka (54), Emmanuel Luhangwa Joseph (40), Yusufu Rajabu Nasoro (20), Zawadi Saimon Ndukeji (27), James Hussein Ntugo (33), Joseph Muyagingwa Englibert (22) na Marco Mahunge Chandanoba (45), ambao wote walipatiwa huduma za awali kabla ya kupelekwa hospitalini kwa matibabu.Majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana (Butimba), huku mmoja wao akihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando kutokana na hali yake kuhitaji matibabu ya kibingwa.Baada ya tukio hilo, eneo la mlipuko lilikaguliwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na Tume ya Madini Mkoa wa Mwanza, ambapo walithibitisha kuwa eneo hilo ni salama na wananchi wanaweza kuendelea kulitumia.Kamanda Mutafungwa ametoa wito kwa viongozi wa serikali za mitaa na wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa kuhusu watu wanaomiliki au kutumia baruti bila vibali halali. Pia amewataka wenyeviti wa mitaa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuwabaini wanaokiuka sheria.Kwa upande wake, Afisa kutoka Tume ya Madini Mkoa wa Mwanza, Deus Makuli, amesema sheria hairuhusu mtu yeyote kumiliki baruti bila leseni, akibainisha kuwa marehemu hakuwa na kibali cha kisheria cha kumiliki vilipuzi hivyo.Makuli amesisitiza kuwa viongozi wa serikali za mitaa wanapaswa kuhakikisha shughuli za ulipuaji wa mawe zinafanywa na watu wenye vibali halali pekee, huku akiwahimiza wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika wanapobaini ukiukwaji wa sheria.Baadhi ya wakazi wa Lwanhima, akiwemo Mahuma Mungu na Adili Atare, wameeleza masikitiko yao kufuatia tukio hilo, wakisema litakuwa fundisho kwa jamii kuhusu hatari ya matumizi na uhifadhi holela wa vilipuzi. Wameahidi kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa dhidi ya watu wanaofanya shughuli za ulipuaji wa mawe bila kufuata taratibu za kisheria.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post