" WATUMISHI WA AFYA HALMASHAURI YA WILAYA MBINGA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

WATUMISHI WA AFYA HALMASHAURI YA WILAYA MBINGA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mbinga Mkoani Ruvuma Joseph Kashushura,akizungumza na baadhi ya watumishi wa kituo kipya cha afya Langiro baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa baadhi ya majengo ya kituo hicho,katikati aliyevaa miwani ni Katibu wa afya wa Halmashauri George Mhina na kulia Mhandisi wa ujenzi Neema Mbilinyi.

Na Mwandishi Maalum, Mbinga

WATUMISHI wa afya Halmashauri ya wilaya Mbinga,wamewatakiwa kuzingatia maadili,weledi,kutoa huduma bora na huruma kwa wagonjwa ili wananchi wavutiwe kwenda kutibiwa kwenye vituo vya afya na hospitali zinazojengwa na Serikali.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Joseph Kashushura,wakati akizungumza na watumishi wapya wa kituo cha afya Langiro kata ya Langiro baada ya kukagua ukamilishaji wa ujenzi wa baadhi ya majengo ya kituo hicho.

Amewataka,kujipanga kwa kutoa huduma bora kwa wagonjwa ili hospitali na vituo vya umma viwe sehemu ya kimbilio,ndiyo maana Serikali imeendelea kuajiri wataalamu wenye sifa wenye jukumu la kutoa huduma kwa weledi na ufanisi mkubwa kwa kuweka mbele uzalendo na huruma kwa wagonjwa.

“Madaktari na wauguzi mnafanya kazi ya kuokoa maisha ya watu na mnayo dhamana ya maisha yetu,Serikali ina matumaini makubwa na nyinyi,hivyo nawaomba fanyeni kazi kwa weledi,tumieni muda wenu kutoa huduma,kuwajali wagonjwa ndiyo msingi wa huduma bora”alisema Kashushura.

Alisema,wakati Serikali inaendelea kuboresha huduma za afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora,ni wajibu kwa kila mtumishi wa sekta ya afya kuhakikisha anatoa huduma sahihi bila upendeleo kwa wagonjwa.

Kashushura alieleza kuwa,iwapo madaktari na wauguzi hawatatoa huduma bora kwa wagonjwa,Serikali itakuwa inapoteza muda kuwekeza fedha nyingi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya,na amewaagiza kufanya kazi zao ili kufikia malengo ya upatikanaji na utoaji wa huduma za afya kwa watanzania.

“Serikali inazifanyia kazi changamoto zote katika sekta ya afya ikiwemo upungufu wa watumishi,hivyo niwaombe licha ya uchache wenu hakikisheni mnatimiza wajibu wenu kwa kutoa huduma za afya kwa mujibu wa viapo vyenu”alisema Kashushura.

Akizungumza na baadhi ya wagonjwa waliofika kupata huduma za matibabu katika kituo hicho,amewataka waendelea kutumia vituo vya afya vya Serikali kwa kuwa vinatoa huduma bora zenye gharama nafuu huku Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya vituo,vifaa tiba na watoa huduma ili kuhakikisha utoaji na upatikanaji wa hudua bora kwa wananchi hasa waishio maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake katibu wa afya wa Halmashauri hiyo George Mhina alisema,wanathamini kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuboresha sekta ya afya na kuhaidi kutoa huduma bora na kutunza miundombinu inayojengwa.

Mkazi wa kijiji cha Langiro Edna Hili,ameishukuru Serikali kuwajengea kituo cha afya na kupata huduma bora ambazo awali walilazimika kwenda kata za jirani kama Litembo na Mbinga mjini kufuata huduma hizo.

“Tunashukuru kupata kituo hiki cha afya kwa kuwa sasa tunapata huduma karibu na nzuri kila tunapofika ikilinganishwa na awali ambapo tulikuwa tunakwenda mbali kwa ajili ya kupata huduma za matibabu”alisema.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post