Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha.
Kampuni ya Hanny G Investment Co. Ltd imeendelea kuhamasisha matumizi ya Jiko Poa, na kuwa suluhisho la kupunguza matumizi ya nishati na kurahisisha shughuli za kupika kwa haraka na kuboresha afya na mazingira.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampuni hiyo iliyopo Kata Kiserian Halmashauri ya Wilaya Arusha, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru, Wazo Mwang'onda amempongeza Mwekezaji wa ndani (Hanny G) Kwa kuunga mkono serikali ya awamu ya sita na Dira ya maendeleo ya taifa 2050 inayotaka kila kaya kutumia nishati safi.
Aidha amesema serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi, hatua inayochochea ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania.
"Matumizi ya nishati safi huupunguza matumizi ya kichochezi cha nishati kwa takribani asilimia 75, jambo linalosaidia kupunguza gharama za kupikia na kuokoa muda.
Mwang'onda amesema kuwa, matumizi ya jiko hilo yanatajwa kupunguza moshi unaotokana na kupikia, hivyo kupunguza hatari ya magonjwa kama nimonia, pumu na kuwashwa kwa macho. na kupunguza uwezekano wa watumiaji kuungua kutokana na joto la moto, na hivyo kuboresha usalama wa watumiaji.
"Uwekezaji huu unaleta faida za kiuchumi na kiafya, Jiko Poa linatajwa kuchangia utunzaji wa mazingira kwa kupunguza uchafuzi wa hewa unaosababisha mabadiliko ya tabianchi na kuhimiza matumizi endelevu ya rasilimali"
Akihitimisha hotuba yake Mwang'onda amesisitiza amani na utulivu kuwa ni msingi wa maendeleo. uwekezaji.Amehimiza kwamba uchumi hauwezi kustawi bila mazingira salama na yenye utulivu.
Kwa upande wake Meneja masoko wa Kampuni hiyo Zera Negro akisoma taarifa ya mradi mbele ya kiongozi wa Mbio za Mwenge amesema mradi huo imetekelezwa Kwa thamani ya shilingi Billions tatu na milions mia tano (3,500,000,0000) hadi kukamilika kwake.
"Kukamilika Kwa mradi huu ni mafanikio makubwa kwetu na jamiii nzima kwani imesaidia kupunguza kuenea hewa ukaa ambayo huchangia kusababisha mabadiliko ya tabia ya nchi" amesema Zera.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment