Naibu Katibu Kitengo cha Elimu ya Sheria kwa Umma Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), Zainabu Chanzi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam Sabasaba Julai 9,2026.
........................
TAFITI zinazofanywa na Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), zimekuwa na mchango mkubwa katika Taifa hasa katika kuanzishwa kwa sheria mpya.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Katibu Kitengo cha Elimu ya Sheria kwa Umma Tume ya
Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), Zainabu Chanzi alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam Sabasaba
Julai 9,2026.
‘’ Tafiti
tunazozifanya zina mchango mkubwa katika taifa kwani baadhi zimeleta sheria
na nyingine zilileta vifungu katika sheria,” alisema Chanzi.
Alisema hapo
awali maendeleo ya kidijitali yalikuwa siyo makubwa lakini yalipokuja Tume hiyo
ilifanya tafiti mwaka 2005 ambayo ilizaa sheria mbili, sheria ya miamala ya
kielektroniki na makosa ya kimtandao.
“Hatukuwa na sheria hizo hivyo baada ya utafiti tulipendekeza Serikalini na ilitunga hizo sheria na ndiyo maana tunaona watu wana udhubutu wa kutuma hela kwa njia ya kimtandao bila ya kuwa na wasiwasi wowote kwa kuwa wanajua zipo sheria,” alisema Chanzi.
Alisema
mwaka 2020 Tume hiyo ilifanya tafiti kuhusiana na ulinzi wa taarifa binafsi
kutokana na kuwa na umuhimu wake kama ambavyo zinavyolindwa katika katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Alisema
katika kuendana na kidijitali Tume imetekeleza wajibu wake na inaendelea na
utekelezaaji huo ambapo kwa sasa inafanya utafiti wa Akili Mnemba (AI) na hayo yote ni mapinduzi yay a kidijitali na
wao kama tume wanazifanya tafiti hizo na kuishauri Serikali iweze kuchukua
hatua zinazofaa kulingana na jamii yetu.
Chanzi
aliongeza kuwa wanaendelea kufanya tafiti na wanapozikabidhi sheria zimekuwa
zikitungwa jambo ambalo wanajivunia.
“Tafiti
tunazo zifanya siyo tu za kidijitali kwa mfano tulifanya teknolojia ya DNA
ambayo zamani ilikuwa haipo lakini Tume ilifanya tafiti na kukabidhi ripoti na
sheria ikatungwa na kwa kuwa tulikuwa na teknolojia lakini bila ya kuiwekea
sheria ya kuisimamia ingeweza kusababisha yasipatikane matokeo chanya ambayo
yangehitajika.
Chanzi
amesema misingi ambayo waliiweka kwenye ripoti zao wameweza kuiona ipo ndani ya
sheria na kuonesha jinsi gani mapendekezo wanayotoa yanavyochukuliwa na
kufanyiwa kazi.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment