
Taasisi mbili za SAT , I am organic wajipanga kupeleka elimu zaidi kwa watanzania Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Wakulima takribani 1000 nchini nzima , wjasiriamali na wafanyabiashara wa kati (SMEs) 50 nchini nzima wamejengewa uwezo kuhusu kilimo hai ambacho hakitumii kemikali na kukuza mnyororo wa thamani kupitia masoko ya wazi kwa bidhaa zinazozalishwa kupitia kilimo hicho ambacho ni salama kwa afya.Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 50 yanayoendelea na Kimataifa ya Biashara kwenye Banda la Wizara ya Kilimo jijini Dar es Salaam yanayoratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) , Afisa Mradi wa SAT, Bw Peter Mwangalo amesema kwamba kwenye maonesho hayo watanzania wanapata fursa ya kujifunza kilimo hai ambacho ni ecolojia ambacho hakitumii kemikali kwenye uandaaji wake.Aliongeza kwamba mradi huo ambao unafadhiliwa na Bio- Vision inaendelea kuwajengea uwezo wafanyabiashara wa kati na wadogo kwa pamoja ili kukuza mnyororo wa thamani na kufungua masoko mapya ya bidhaa zinazotokana na kilimo hai nchini kupitia pia viwanja vya saba saba.“Mradi huo wa miaka minne unaofadhiliwa na shirika la kimataifa la Bio- Vision la nchini Uswisi ina lengo la kuhakikisha wakulima, wafanyabiashara na wajasirimali wanapata uelewa wa pamoja, mafunzo na mbinu za kufanya kilimo hai bila kutumia mbolea zenye sumu,” alisema Bw Mwangalo Aliongeza kwamba kilimo hai ina manufaa makubwa sana kwa watanzania kwa sababu hakitumii mbolea zenye sumu , kemikali na aina zingine za madawa isipokuwa njia za asili ambazo ni rafiki kwa mazingira na bora za zaidi kwa afya ya watanzania.Mwangalo alisisitiza kamba ni muhimu kwa watanzania wadau mbalimbali kuendelea kutembelea banda hilo kujifunza bidhaa za kilimo hai ambazo zinapatikana pia kwenye viwanja hivyo vya sabasaba.Kwa upande wake , Meneja wa Duka la (I am organic) , Bi Dainess Sunday amesema kwamba bidhaaa hizo za kilimo hai kutumia mbinu za kilimo za ikolojia ambazo ni rafiki pia kwa mazingira , bionuai na kulinda afya za walaji na wazalishaji.Alisema kwamba lengo la mradi huo ni kuendelea kuwajengea uwezo watanzania ambao ni wakulima , wafanyabiashara na wajasiriamali kujua umuhimu wa bidhaa hizo za kilimo hai na kukuza mnyororo wa thamani.Aliongeza kwamba bidhaa zinazotokana na kilimo hai zinawafanya walaji kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kama vile kansa za aina zote ambayo magonjwa hayo kwa kiasi kikubwa yanatokana na mtindo wa maisha ya kila siku.“Tunafungua furs ana milango kwa wakulima wa mazao ya kilimo hai kuweza kupata masoko ndani ya nchini na nje lakini pia kusambaza ujumbe na elimu ya kilimo hai kwa afya za binadamu na uchumi wa watanzania kwa ujumla,” alisema Bi Sunday Naye Bi Aslatu Nguku kutoka Mama Health Organic shop , Dodoma mmoja wa wanufaika wa mafunzo ya kilimo hai kupitia mradi huo amesema kwamba kilimo hicho kinachangia kwa kiasi kikubwa harakati za utunzaji wa mazingira kutoka na mbinu zinazotumika.“kwa kiasi kikubwa ongezeko la matumizi ya bidhaa zinazotokana na kilimo hai nchini zinaendelea kuongeza kwa kasi kwenye mikoa mbalimbali nchini nzima,” alisema Bi NgukuMradi huo wa miaka minne unaofadhiliwa na shirika la Kimataifa la Bio – vision la nchini Uswisi ambapo limetokea kiasi cha shilingi za kitanzania 1.2 billioni ili kuhakikisha wakulima, wafanyabiashara na wajasiiamali wanapata uelewa , mafunzo na mbinu za kufanya kilimo hai bila kutumia mbolea zenye sumu.Mradi huo zimefanikiwa kuwafikia wajasiriamali na wafanyabiashara wa kati na wadogo kutoka sehemu za Morogoro, Dar es Salaam, Njombe, Lindi , Iringa, Arusha na Kagera kwa kuwapa mafunzo, taarifa na kuhamasisha kilimo hai kwa manufaa ya mazingira na afya kwa walaji.kilimo hai ni kilimo ambacho kina fursa ya kuboresha afya za watanzania na kudhibiti magonjwa mmbalimbali ikiwemo magonjwa ya moyo na ngozi na ni rafiki kwa mazingira.Mwisho SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment