" AMANI NI URITHI MKUBWA WA TANZANIA : DKT. BITEKO

AMANI NI URITHI MKUBWA WA TANZANIA : DKT. BITEKO





Amani ni urithi mkubwa wa Tanzania na msingi wa maendeleo yanayoendelea kushuhudiwa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko, wakati wa ibada na mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ilolangulu, Kabula Ndabacha, yaliyofanyika wilayani Mbogwe mkoani Geita.



Kutokana na haja hiyo amewataka Watanzania kuendelea kuenzi na kuudumisha utamaduni huo wa upendo, umoja na mshikamano akisisitiza kuwa misingi hiyo ni nguzo muhimu ya maendeleo endelevu ya Taifa.

Dkt. Biteko amesema nyakati za mafanikio na changamoto zinahitaji wananchi kuendelea kuthaminiana, kusaidiana na kuishi kwa upendo bila kujali tofauti zao. Aidha, ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema kifo cha Ndabacha ni pigo kubwa kwa familia, wananchi wa Kata ya Ilolangulu na chama hicho kutokana na mchango wake katika kuwatumikia wananchi.

Amewataka wananchi wote kuendeleza mema yote yaliyoachwa na marehemu kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo, kuimarisha mshikamano na kulinda amani ambayo imekuwa tunu na fahari ya Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post