" CHATANDA: TAMASHA LA KIZIMKAZI LINACHOCHEA UPENDO, MSHIKAMANO NA MAENDELEO

CHATANDA: TAMASHA LA KIZIMKAZI LINACHOCHEA UPENDO, MSHIKAMANO NA MAENDELEO

 


NA: MWANDISHI WETU, ZANZIBAR 

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Mary Chatanda, ameungana na viongozi na wananchi katika Tamasha la Kizimkazi katika mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Akizungumzia tamasha hilo,  Agosti 13, 2026, Chatanda amesema, linasaidia kukuza upendo, mshikamano na maendeleo miongoni mwa viongozi na wananchi, hivyo linapaswa kuendelezwa. 

"Tamasha la Kizimkazi linawaleta watu pamoja kutoka maeneo tofauti nchini, hili ni jambo kubwa sana, tunaongea na kubadilishana mawazo. Pia, miradi ya maendeleo kama ya elimu, afya, maji inazinduliwa katika kutatua kero za wananchi," amesema Chatanda.

Aidha, amepongeza suala la utamaduni kuenziwa katika tamasha hilo, kwani utamaduni una umuhimu mkubwa katika kuliheshimisha taifa na kukuza maendeleo.


"Upekee mwingine wa tamasha hili ni kuenzi utamaduni wetu yaani mavazi, vyakula, ngoma za asili, lugha yetu ya Kiswahili, tukumbuke kuwa utamaduni unaibua fursa za kiuchumi katika kuongeza kasi ya maendeleo," amesisitiza.

Katika tamasha hilo, Chatanda ameshiriki uzinduzi na ukaguzi wa mradi wa Makaazi wa Amani (Amani Residency) na upandaji miti katika Kituo cha Afya Kizimkazi.

Viongozi mbalimbali wakiwemo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Dk. Hussein Mwinyi, mawaziri, wabunge, viongozi wa Chama, serikali na wananchi mbalimbali wameshiriki tamasha hilo ambalo linagusa nyanja zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa katika kukuza maendeleo nchini.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 









Post a Comment

Previous Post Next Post