" WANANCHI WAIPONGEZA POLISI JAMII TINGI MISSION NYASA.

WANANCHI WAIPONGEZA POLISI JAMII TINGI MISSION NYASA.



Wananchi wa Kata ya Tingi Tarafa ya Mpepo Wilaya ya Nyasa wamelipongeza Jeshi la Polisi  kwa huduma wanayoipata.

Jeshi la Polisi kupitia mpango wa Polisi Jamii limeendelea kuimarisha uhusiano na jamii kwa kutoa elimu  ya usalama, ulinzi na ushirikiano kwa watu wazima,  wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi Tingi Mission na Kibaoni, Kata ya Tingi, Tarafa ya Mpepo , Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma.

Elimu hiyo imetolewa na Mkaguzi wa Polisi Kata ya Tingi, INSP. Juma Rashid Mbwana, ambapo wanafunzi wa Darasa la Saba wa shule hizo mbili pamoja na walimu 78 walinufaika na ujumbe uliolenga kuwajenga kuwa na nidhamu, uwajibikaji na uelewa wa masuala ya usalama.

Katika utekelezaji wa mpango wa "Outreach Program", Polisi Jamii pia ilitoa motisha kwa wanafunzi watatu kwa kutambua juhudi zao katika mitihani ya Mock ya Mkoa wa Ruvuma mwaka 2026 ambapo  Moja ya wanafunzi ambao ni  Deo Nyoni na Modesta Mapunda walipongezwa kwa kufanya vizuri na kupewa zawadi kama hamasa ya kuendelea kujituma.

Aidha, mwanafunzi Philbert Kawonga ambaye hakufanya vizuri katika mitihani hiyo pia alipewa motisha maalumu na nasaha ili asikate tamaa, bali kuongeza bidii katika masomo yake.

Hatua hiyo imeonyesha kuwa Polisi Jamii  kupitia Insp. Juma Mbwana si chombo cha ulinzi na usalama pekee, bali pia ni mshirika katika malezi, elimu na maendeleo ya jamii. 


Wanafunzi walihimizwa kuthamini elimu, kuheshimu wazazi na walimu, kuwa na nidhamu na kushirikiana na vyombo vya usalama.

Tukio hilo limepokelewa kwa furaha na jamii ya Tingi Mission  pia kwa wana mitandao mkoani Ruvuma huku likiongeza morali kwa wanafunzi kusoma kwa bidii na kuamini kuwa kila mmoja ana uwezo wa kufikia mafanikio kupitia juhudi.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 








Post a Comment

Previous Post Next Post