" DIB YAWAHIMIZA WANANCHI KUWEKA AKIBA KWENYE TAASISI ZENYE LESENI

DIB YAWAHIMIZA WANANCHI KUWEKA AKIBA KWENYE TAASISI ZENYE LESENI

 Bodi ya Bima ya Amana (DIB) imewataka wananchi kutumia fursa ya Maonesho ya Nanenane kutembelea banda la DIB ili kupata elimu kuhusu ulinzi wa amana zao na taratibu za kufidia fedha wanazoweka katika taasisi za fedha zenye leseni ya Benki Kuu ya Tanzania.

Akizungumza katika Maonesho ya kimataifa ya wakulima ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni, Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Bima ya Amana Isack Kihwila amewasisitiza wananchi kuweka fedha zao katika benki na taasisi za fedha zilizosajiliwa na kupewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania, akionya kuwa kuweka fedha katika taasisi zisizo rasmi kunaweza kuwanyima haki ya kufidiwa endapo taasisi hizo zitashindwa kutekeleza majukumu yake.

Sambamba na hayo Kihwila imewataka wenye amana wa iliyokuwa Benki ya FBME ambao bado hawajachukua fedha zao kujitokeza haraka ili kukamilisha mchakato wa malipo, ikieleza kuwa mabilioni ya fedha bado yanawasubiri walengwa.

lisema taasisi hiyo imefikia hatua kubwa ya kulipa madai ya wenye amana, huku ikisalia asilimia ndogo ya walengwa ambao hawajajitokeza.

Alisema madai ya wenye amana wa Benki ya FBME kwa upande wa Tanzania yalifikia takribani shilingi bilioni 35, na hadi sasa zaidi ya asilimia 85 ya fedha hizo tayari zimelipwa kwa walengwa.

Aidha Mkurugenzi huyo, bado kuna takribani watu 428 ambao hawajajitokeza kuchukua fedha zao, zenye thamani ya karibu shilingi bilioni nne, licha ya fedha hizo kuwa tayari zimetengwa kwa ajili yao.

Alifafanua kuwa baada ya kundi hilo kujitokeza na kulipwa fedha zilizokuwa zimeshatengwa, hatua inayofuata itakuwa ni kulipa asilimia 15 zilizobaki ili kila mwenye amana astahili kulipwa madai yake kwa asilimia 100.

Aidha, alisema bado kuna kundi la wadai wengine, wakiwemo baadhi ya wafanyakazi waliokuwa na madai yaliyofikishwa mahakamani, ambao malipo yao hayajahusishwa katika awamu inayoendelea kutokana na mchakato wa kuendelea kufuatilia na kuhakiki mali za benki hiyo.

Alisema DIB inaendelea kufanya kazi ya kufuatilia mali zilizobaki ili kuhakikisha fedha za kutosha zinapatikana kwa ajili ya kukamilisha malipo ya wadai hao kwa kuzingatia taratibu za kisheria.        

Post a Comment

Previous Post Next Post