" HATIBU MGEJA AKABIDHIWA RASMI OFISI YA RED CROSS MKOA WA SHINYANGA

HATIBU MGEJA AKABIDHIWA RASMI OFISI YA RED CROSS MKOA WA SHINYANGA

Mwenyekiti mpya wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) Mkoa wa Shinyanga, Hatibu Madata Mgeja, amekabidhiwa rasmi ofisi pamoja na mali za taasisi hiyo, ikiwa ni hatua ya kuanza rasmi majukumu yake baada ya kuchaguliwa kuongoza chama hicho mkoani Shinyanga.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Agosti 17, 2026 katika Ofisi za TRCS Mkoa wa Shinyanga, ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa Red Cross Mkoa wa Shinyanga, Robert Kayoka, amekabidhi ofisi na mali za taasisi kwa Mwenyekiti mpya.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekiti mpya, Hatibu Madata Mgeja, amesema amepokea dhamana hiyo kwa heshima na atashirikiana na viongozi, wanachama, Serikali pamoja na wadau mbalimbali katika kuimarisha shughuli za Chama cha Msalaba Mwekundu Mkoa wa Shinyanga.

Mgeja amesema uongozi wake utalenga kuimarisha ushirikiano na wadau pamoja na kuhakikisha shughuli za chama zinawafikia wananchi wenye uhitaji, huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano katika kutekeleza majukumu ya kibinadamu.

Makabidhiano hayo yamehitimisha rasmi kipindi cha uongozi wa Robert Kayoka na kufungua ukurasa mpya wa uongozi chini ya Mwenyekiti Hatibu Madata Mgeja, ambaye anatarajiwa kuendelea kuimarisha utendaji na huduma za Chama cha Msalaba Mwekundu Mkoa wa Shinyanga.

Makabidhiano rasmi ya Ofisi na Mali za Red Cross Mkoa wa Shinyanga, ambapo Mwenyekiti mpya Hatibu Madata Mgeja (kulia) akikabidhiwa rasmi ofisi na mali za taasisi na aliyekuwa Mwenyekiti Robert Kayoka.




 

Post a Comment

Previous Post Next Post