Kampuni ya Neerika Oil iliyopo Nyarugusu wilayani Geita imetoa ofa ya punguzo la bei kwa huduma zake kwa siku tatu baada ya kufunguliwa kwa kituo chake na mbio za mwenge.
Meneja wa Kampuni hiyo ambaye pia ni Mhasibu John Masenga alisema ofa hiyo ya punguzo la bei ya mafuta imeenda sambamba na utolewaji wa reflectors na helmet kwa bodaboda.
Alisema hatua hiyo ni mojawapo ya kuifanya jamii iliyowazunguka kuelewa huduma zao hizo wanazotoa hivyo waweze kutumia katika utendaji kazi zao za kila siku.
Masenga aliishukuru serikali kwa ushirikiano inaotoa kwao wawekezaji wazalendo na hivyo kuomba hali hiyo kudumishwa kwa manufaa ya taifa.
Aidha ameomba wafanyabiashara katika eneo la Nyarugusu kutoa ushirikiano kwao kwani huduma hiyo ya kituo cha mafuta imejengwa na kampuni hiyo ambayo ni wadau kwenye sekta ya madini ili kuondoa adha ya kwenda mbali kupata huduma hiyo.

Mradi huo uliogharimu zaidi ya sh milioni 400 unamilikiwa na Richard Kasubi ambaye anathamini uzalendo unaofanywa ya uzinduzi wa miradi ya maendeleo kupitia mbio za mwenge.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Uhuru Kitaifa mwaka huu Wazo Mwan'gonda aliipongeza kampuni hiyo ya kizalendo kwa uwekezaji huo ilioufanya.
Alisema kwa serikali ni faraja kubwa kuona kuwa wawekezaji wazalendo wana jitokeza kwa wingi kusaidia jamii kuweza kupata mahitaji kwa ukaribu.
Mwang'onda alisema serikali ya Awamu ya sita itaendelea kujenga mazingira wezeshi kuwezesha ukuaji wa sekta binafsi hapa nchini.

Ofisa Usafirishaji wa eneo la Nyarugusu Elia Paul alipongeza kupatikana kwa punguzo kwa huduma za mafuta katika sehemu hiyo.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment