" .KAULI YA MEYA YALETA MATUMAINIYAKUPUNGUZAMSONGAMANO JIJINI ARUSHA

.KAULI YA MEYA YALETA MATUMAINIYAKUPUNGUZAMSONGAMANO JIJINI ARUSHA

Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha.

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maxmillian Iranqhe ametoa kauli ya matumaini ya kuondoa msongamano Jijini Arusha iwapo itafanyiwa kazi.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake amesema magari yanapoingia sokoni yatanatakiwa yashushe mizigo na kuondoka Ili kupisha wanunuzi kupata mahali pa kuegesha magari yao.

Aidha amewataka Meneja wa masoko yote yaliyopo Jijini kusimamia suala hilo kikamilifu, na kuhakikisha hakuna bidhaa zinazouzwa ndani ya gari sokoni. Hata hivyo amemtaka kila mmoja kufuata Sheria ili kuliweka Jiji safi.

Katika namna hiyo hiyo Meya amesema tayari mkataba wa kufunga taa 500 za barabarani wenye thamani ya shilingi Billions 2 umesainiwa Kwa lengo la kuona wananchi wanafanya biashara usiku na mchana.

Ametoa rai Kwa Mkandarasi aliyesaini mkataba kufunga taa hizo kuwa mwamimifu  Kwa kufunga taa imara na kukamilisha kazi hiyo Kwa wakati.

"Uwekaji taa za barabarani unaendelea kulingana na umuhimu wa eneo husika lakini matarajio yetu ni kuona kila eneo katika Jiji hili linawaka taa, hatua hiyo itasaidia wafanyabiashara kufanya kazi zao mchana na usiku"amesema Iranqhe.

Vilevile ametoa rai Kwa Machinga wote Jijini Arusha kufanyia biashara katika maeneo waliyopangiwa, na si kukaa barabarani.

Mh. Meya amesema kila mmoja atakayekiuka taratibu za kufanyia biashara eneo alilopangiwa sheria itafuata mkondo wake. Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maxmillian Iranqhe ametoa kauli ya matumaini ya kuondoa msongamano Jijini Arusha iwapo itafanyiwa kazi.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake amesema magari yanapoingia sokoni yatanatakiwa yashushe mizigo na kuondoka Ili kupisha wanunuzi kupata mahali pa kuegesha magari yao.

Aidha amewataka Meneja wa masoko yote yaliyopo Jijini kusimamia suala hilo kikamilifu, na kuhakikisha hakuna bidhaa zinazouzwa ndani ya gari sokoni. Hata hivyo amemtaka kila mmoja kufuata Sheria ili kuliweka Jiji safi.

Katika namna hiyo hiyo Meya amesema tayari mkataba wa kufunga taa 500 za barabarani wenye thamani ya shilingi Billions 2 umesainiwa Kwa lengo la kuona wananchi wanafanya biashara usiku na mchana.

Ametoa rai Kwa Mkandarasi aliyesaini mkataba kufunga taa hizo kuwa mwamimifu  Kwa kufunga taa imara na kukamilisha kazi hiyo Kwa wakati.

"Uwekaji taa za barabarani unaendelea kulingana na umuhimu wa eneo husika lakini matarajio yetu ni kuona kila eneo katika Jiji hili linawaka taa, hatua hiyo itasaidia wafanyabiashara kufanya kazi zao mchana na usiku"amesema Iranqhe.

Vilevile ametoa rai Kwa Machinga wote Jijini Arusha kufanyia biashara katika maeneo waliyopangiwa, na si kukaa barabarani.

Mh. Meya amesema kila mmoja atakayekiuka taratibu za kufanyia biashara eneo alilopangiwa sheria itafuata mkondo wake.

Post a Comment

Previous Post Next Post