
Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ndg. Evarist Simon Mnyere, ikifanya ziara ya kikao katika Wilaya ya Mpanda tarehe 18/09/2026.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi, Evarist Simon Mnyere, amefanya kikao na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mpanda pamoja na wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Kata zote 27 za Wilaya ya Mpanda, kwa lengo la kuimarisha jumuiya, kusikiliza na kutatua kero za wanachama pamoja na kuhimiza maendeleo ya kisiasa na kijamii.
Kikao hicho kilifanyika Septemba 18, 2026, ambapo Mnyere alikutana na viongozi hao kwa ajili ya kuwasalimia, kuwashukuru na kuwapongeza kwa mchango wao katika kufanikisha shughuli za chama.
Katika kikao hicho, Mnyere aliwashukuru wajumbe hao kwa ushiriki wao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, sambamba na kuwapongeza wanachama kwa mchango wao uliochangia kufanikisha ushindi wa Chama Cha Mapinduzi katika nafasi mbalimbali za udiwani, ubunge na urais.
Alisema ushindi huo unatokana na mshikamano na juhudi za pamoja, hivyo akawahimiza viongozi na wanachama kuendelea kudumisha umoja na mshikamano kwa ajili ya maendeleo ya jumuiya na jamii kwa ujumla.
Mnyere pia alisisitiza umuhimu wa kuendelea kudumisha upendo na amani, akieleza kuwa ni misingi muhimu katika ujenzi wa taifa lenye utulivu.
Aidha, aliwataka viongozi wa Jumuiya ya Wazazi katika ngazi mbalimbali kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kuzingatia maslahi ya wananchi, huku akiwakumbusha wanajumuiya kushiriki kikamilifu katika shughuli za jumuiya na kuhakikisha ada za uanachama zinalipwa kwa wakati.
Katika hatua nyingine, Mnyere alizitaka Kamati za Utekelezaji za Wilaya na Kata zote 27 za Mpanda kusimamia maendeleo katika maeneo yao na kushirikiana kwa karibu na wanachama bila ubaguzi.
Alisisitiza umuhimu wa viongozi kufanya ziara na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi ili kuleta matokeo chanya kwa wananchi na wanachama, pamoja na kubuni miradi ya maendeleo itakayopanua fursa za kiuchumi katika maeneo yao.
Mwenyekiti huyo pia aliwataka viongozi wa ngazi mbalimbali kuhakikisha wanakuwa na takwimu sahihi za wanachama, kufanya vikao vya mara kwa mara, kutunza kumbukumbu na kusikiliza pamoja na kutatua kero za wanachama kwa wakati.
Ziara hiyo ilihitimishwa kwa maelekezo kwa viongozi wa ngazi za mashina, matawi, kata na wilaya kuendelea kusimamia majukumu yao kwa uwajibikaji, huku wakisisitizwa kuendelea kubuni miradi ya maendeleo, kuimarisha mawasiliano na kujenga mahusiano mazuri kati ya chama na Serikali kwa kila kiongozi kutekeleza wajibu wake kulingana na nafasi aliyonayo.

Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda na mwakilishi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, tarehe 18/09/2026 alishiriki kikamilifu katika kikao cha kupokea ugeni wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi, iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi, Ndg. Evarist Simon Mnyere.

Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, akiwa mwenyeji wa ugeni huo na mwakilishi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, ameshiriki kikamilifu katika ziara ya kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi, iliyofanyika tarehe 18/09/2026.

Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi, Ndg. Evarist Simon Mnyere, pamoja na wenyeviti wa Jumuiya ya Wazazi wa Kata zote 27 za Wilaya ya Mpanda, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara ya kikao hicho iliyofanyika tarehe 18/09/2026.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment