
Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Nuhu Mruma wamewataka Watanzania kudumisha amani, umoja, upendo na maadili mema.
Aidha alihimiza matumizi sahihi ya teknolojia na mitandao ya kijamii ili kuepuka kueneza taarifa za uongo, matusi na maudhui yasiyozingatia maadili.
Alisema hayo katika Baraza la Maulid la Kitaifa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam jana.
Alisema ni muhimu Watanzania kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii. Alitaja miongoni mwa changamoto ni picha zisizo na maadili, matusi dhidi ya watu na viongozi na kusambaza taarifa za uongo zinazoweza kusababisha taharuki katika jamii.
Aliomba vyombo vinavyohusika na usimamizi wa Sheria ya Makosa ya Mitandao ya Mwaka 2015 kuendelea kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao ili kupunguza uhalifu wa mtandaoni.
Mruma pia alisisitiza umuhimu wa amani na mahusiano mema katika jamii, akisema mafundisho ya Mtume Muhammad yanahimiza kuishi vizuri na majirani bila kujali tofauti za dini. Alitangaza kuwa maandalizi ya hija ya mwaka 2027 yameanza rasmi, huku uandikishaji wa mahujaji ukiendelea kupitia Idara ya Hija na Umrah ya Bakwata, pamoja na ofisi za mikoa na wilaya.
Alisema gharama ya hija kupitia Bakwata kwa mwaka 2027 ni Dola za Marekani 6,300 sawa na takribani Sh milioni 16.7, kutegemea thamani ya Dola kwa siku husika. Mruma aliwataka Waislamu wanaokusudia kwenda hija mwakani kuanza taratibu za usajili mapema kutokana na mabadiliko ya mifumo na muda wa mwisho wa usajili unaowekwa na Wizara ya Hija na Umrah ya Saudi Arabia.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye pia anakaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira ya utulivu na amani yanayowawezesha wananchi wa dini mbalimbali kufanya ibada zao bila changamoto.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Faustine Furaha alisema mwaliko wa viongozi wa dini nyingine katika Baraza la Maulid ni ushahidi kwamba Tanzania ni nyumba moja na wananchi wake ni watoto wa Mungu mmoja.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment