Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwenge wa
Uhuru ukiongozwa na Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Wazo Marco Mwang’onda, umeendelea
na shughuli zake katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kuzindua,
kuweka mawe ya msingi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani
ya zaidi ya shilingi bilioni 5.2.
Katika ziara
hiyo, Mwenge wa Uhuru umefikia miradi mbalimbali katika sekta za afya, maji,
elimu, nishati, uwezeshaji wananchi kiuchumi na miundombinu, ambapo mwenge wa
uhuru umetamka kuwa miradi hiyo imekidhi
viwango na imepitishwa kwa ajili ya matumizi ya wananchi.
Akizungumza
wakati wa hafla hizo, Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Wazo Marco Mwang’onda, amesema
Mwenge wa Uhuru unaendelea kuwa chombo muhimu katika kuhamasisha wananchi
kushiriki katika shughuli za maendeleo, kusimamia matumizi sahihi ya fedha za
umma na kuhakikisha miradi inayotekelezwa inawanufaisha wananchi.
Amesema
ziara hiyo inalenga pia kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kutunza na kutumia
vizuri miradi inayotekelezwa kwa fedha za Serikali pamoja na kuendelea
kushirikiana na viongozi katika kusukuma mbele maendeleo ya maeneo yao.
Katika ziara
hiyo, Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa maji safi katika Kitongoji cha Mwamala,
ukiwa ni miongoni mwa miradi inayolenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji
kwa wananchi wa eneo la kata ya Kolandoto.
Mwenge pia
umefungua mradi wa Zahanati ya Mwagala, iliyopo Kata ya Ibadakuli, wenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa zahanati hiyo, Mwang’onda ameeleza umuhimu wa uwepo wa
huduma za afya karibu na wananchi, huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan
kwa kuendelea kuimarisha miundombinu ya afya nchini.
Baadhi ya
wananchi wa Mwagala wameishukuru Serikali kwa kuhakikisha mradi huo unakamilika
na kuanza kutoa huduma kwa jamii.
Katika hatua
nyingine, Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi katika Makindo Hotel, mradi
ambao ni miongoni mwa uwekezaji unaolenga kuchochea shughuli za kiuchumi na
kuongeza fursa za ajira na biashara katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenge pia
umefikia Kikundi cha Mkasa Fashion, kinachoundwa na vijana ambao ni wanufaika
wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga.
Aidha,
Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa nishati safi ya kupikia, unaosimamiwa na
Taasisi ya Wanawake na Samia Mkoa wa Shinyanga, ukiwa na lengo la kuhamasisha
matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia.
Katika sekta
ya miundombinu Mwenge wa uhuru umeweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa
Daraja la Dodoma, lililopo Kata ya Ndembezi na kwamba mradi huo una thamani ya
zaidi ya shilingi milioni 100.
Mwenge pia
umetembelea na kukagua ukarabati wa vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya
Sekondari Old Shinyanga, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na
kufundishia kwa wanafunzi.
Katika
shughuli hizo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Shinyanga Mjini, Paschal Patrobas Katambi, ameshiriki katika shughuli za
mapokezi na ufuatiliaji wa ziara ya Mwenge wa Uhuru, akisisitiza umuhimu wa
Serikali na wananchi kuendelea kushirikiana katika kuleta maendeleo.
Mwenge wa
Uhuru unaendelea na shughuli zake mkoani Shinyanga, ambapo unatarajiwa
kuendelea na ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, huku ukibeba
kauli mbiu inayosema:
“TANZANIA NI YETU SOTE, TUSHIKAMANE KWA PAMOJA KULETA MAENDELEO.”
Mwenge wa Uhuru ukibebwa na kukimbizwa na watu mbalimbali wakati ukiendelea na shughuli zake katika Manispaa ya Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya mbio za kuhamasisha amani, mshikamano na maendeleo.
Mwenge wa Uhuru ukibebwa na kukimbizwa na watu mbalimbali wakati ukiendelea na shughuli zake katika Manispaa ya Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya mbio za kuhamasisha amani, mshikamano na maendeleo.
Mwenge wa Uhuru ukibebwa na kukimbizwa na watu mbalimbali wakati ukiendelea na shughuli zake katika Manispaa ya Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya mbio za kuhamasisha amani, mshikamano na maendeleo.
Mwenge wa Uhuru ukibebwa na kukimbizwa na watu mbalimbali wakati ukiendelea na shughuli zake katika Manispaa ya Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya mbio za kuhamasisha amani, mshikamano na maendeleo.
Mwenge wa Uhuru ukibebwa na kukimbizwa na watu mbalimbali wakati ukiendelea na shughuli zake katika Manispaa ya Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya mbio za kuhamasisha amani, mshikamano na maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akizungumza wakati wa ziara ya Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Manispaa ya Shinyanga.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Paschal Patrobas Katambi, akizungumza wakati wa ziara ya Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Manispaa ya Shinyanga.
Taarifa ya mradi wa Zahanati ya Mwagala.
Mwenge wa Uhuru umefungua Zahanati ya Mwagala, Kata ya Ibadakuli, yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100, ikiwa ni hatua ya kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.
Mwenge wa Uhuru umefungua Zahanati ya Mwagala, Kata ya Ibadakuli, yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100, ikiwa ni hatua ya kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wazo Marco Mwang’onda, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Zahanati ya Mwagala, Kata ya Ibadakuli, Manispaa ya Shinyanga.
Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa maji safi katika Kitongoji cha Mwamala, Manispaa ya Shinyanga, hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi.
Mwenge wa Uhuru umefikia Kikundi cha Mkasa Fashion, kinachonufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wazo Marco Mwang’onda, akizungumza wakati wa kutembelea na kukagua shughuli za Kikundi cha Mkasa Fashion, kinachonufaika na mkopo wa asilimia 10 wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa nishati safi ya kupikia unaosimamiwa na Taasisi ya Wanawake na Samia Mkoa wa Shinyanga, ukiwa na lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati salama na rafiki kwa mazingira.
Peter Joseph, mwakilishi wa Shirika la Youth and Women Emancipation (YAWE), akiwa upande wa kulia, akipokea cheti kwa niaba ya shirika hilo kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wazo Marco Mwang’onda, kwa kutambua mchango wa YAWE katika utunzaji wa mazingira Shinyanga.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wazo Marco Mwang’onda, akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa Daraja la Dodoma
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wazo Marco Mwang’onda, akizungumza wakati wa kutembelea na kukagua ukarabati wa vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya Sekondari Old Shinyanga.

Burudani.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254









































Post a Comment