Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imelipatia cheti Shirika la Youth and Women Emancipation (YAWE) kwa kutambua mchango wake katika shughuli za utunzaji na uhifadhi wa mazingira.
Cheti hicho
kimetolewa kwa YAWE ikiwa ni miongoni mwa wadau wanaofanya vizuri katika
kuhamasisha na kutekeleza shughuli zinazolenga kulinda mazingira katika
Manispaa ya Shinyanga.
Cheti hicho
kimekabidhiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wazo Marco Mwang’onda,
mara baada ya hafla ya uzinduzi wa mradi wa nishati safi ya kupikia
unaotekelezwa kata ya Ndembezi.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo, Wazo Marco Mwang’onda ameupongeza uongozi wa YAWE kwa
jitihada za kushiriki katika shughuli za utunzaji wa mazingira, akisisitiza
umuhimu wa wadau kuendelea kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na
changamoto za uharibifu wa mazingira.
Amesema
matumizi ya nishati safi ya kupikia ni miongoni mwa hatua muhimu katika kulinda
mazingira, kupunguza utegemezi wa nishati zinazochangia uharibifu wa misitu na
kuboresha afya za wananchi.
Mwakilishi
wa shirika la YAWE Bwana Peter Joseph
ameishukuru Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kutambua mchango wa
shirika hilo, huku ukieleza kuwa cheti hicho ni motisha ya kuendelea kuimarisha
shughuli za utunzaji wa mazingira na kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa
matumizi ya nishati safi.
Hatua hiyo
imekuja wakati ambapo Mwenge wa Uhuru 2026 ukiendelea na shughuli zake mkoani
Shinyanga, ukiwa na kauli mbiu inayosema: “Tanzania ni yetu sote, tushikamane
kwa pamoja kuleta maendeleo.”
Peter Joseph, mwakilishi wa Shirika la Youth and Women Emancipation (YAWE), akiwa upande wa kulia, akipokea cheti kwa niaba ya shirika hilo kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wazo Marco Mwang’onda, kwa kutambua mchango wa YAWE katika utunzaji wa mazingira Shinyanga.
Peter Joseph, mwakilishi wa Shirika la Youth and Women Empowerment (YAWE), akiwa upande wa kulia, akipokea cheti kwa niaba ya shirika hilo kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wazo Marco Mwang’onda, kwa kutambua mchango wa YAWE katika utunzaji wa mazingira Shinyanga.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment