Mkufunzi
wa mafunzo ya mameneja wa vituo vya Radio mikoa mitatu ya kanda ya Ziwa
Nuzulack Daussen ambae pia ni Mtendaji wa Taasisi ya Nukta Afrika amempongeza
ripota wa Gold Fm manispaa ya Shinyanga Mapuli Misalaba kwa utengenezaji wa
maudhui ya uigizaji (SHY TALENT FILMS) ambayo amesema huenda yakamuongezea
mapato siku zijazo
Ripota huyo anaemiliki Misalaba Media amepongezwa kwa ubunifu wa maudhui hayo
ambayo mkufunzi huyo amesema Yana maslahi katika Dunia hii ya teknolojia.
Akizungumza katika mafunzo ya mameneja wa vituo vya Radio mikoa mitatu ya kanda
ya Ziwa ambayo ni Shinyanga,Mwanza na Geita amesema Dunia ya teknolojia bila
kuwa mbunifu wa maudhui na kutumia platform za dijitali unaweza usifikie
malengo.
Mafunzo hayo ambayo yamefadhiliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania Kanda ya
Ziwa ni ya kuwawezesha mameneja wa vituo vya Radio katika mikoa hiyo mitatu
kujitegemea na kutengeneza mapato zaidi.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum Banali akifungua mafunzo
hayo amesema ni wajibu wa kila kituo cha utangazaji kuwapatia mafunzo staff wao
ambapo amesema hilo ni takwa la kisheria katika utangazaji.
Katika mafunzo hayo mameneja wa vituo vya Radio kutoka mikoa hiyo mitatu pia
walijifunza kutengeneza mipango kazi katika vyumba vya habari,kutumia platform
za dijitali kuongeza mapato na kutengeneza mpango kazi katika biashara.
Mameneja hao pia walitumia nafasi hiyo kujadili changamoto mbalimbali katika
eneo la biashara na maudhui.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
Post a Comment