Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Janeth Magomi ameongoza matembezi ya kuadhimisha kilele cha maadhimisho ya mika ishirini ya Polisi Jamii.Akizungumza baada ya matembezi hayo SACP Magomi aliwashukuru askari na wananchi waliojitokeza katika matembezi hayo na kuwaalika katika chakula cha mchana na matendo ya huruma yaliyoandaliwa kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Buhangija.Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Fraterine Tesha alihimiza kuishi kauli mbiu ya Polisi Jamii ambayo ni *KUDUMISHA AMANI NA USALAMA* kwani jamii yenye amani na usalama inakuwa na fursa mbalimbali za kiuchumi na maendeleo hushamiriNao wanakikundi wa Polisi Jamii Fitness Centre waliunga mkono jambo hilo kwa kutoa michango yao kwa ajili ya kuwapa faraja watoto hao ili waweze kupata mahitaji mbalimbali.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment