Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu ametoa wito kwa waumini wa dini ya kiislamu kuyashika na kuyaishi kwa vitendo mafundisho na Maisha ya Mtume Mohammad (S.A.W) hususan katika kuimarisha maadili, upendo, amani na mshikamano katika jamii ili kujenga Taifa lenye maadili mema na uwajibikaji.
Aidha ametaka kuendelezwa kwa ushirikiano wa taasisi za kidini na Serikali ili kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano, akisisitiza kuwa misingi hiyo ni nguzo muhimu katika kujenga Taifa imara.
Mhe. Sangu ametoa wito huo Jumapili, Agosti 30, 2026) alipomwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba katika hafla ya kumbukizi ya mazazi ya Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam) yaliyofanyika katika uwanja wa Kigogo Posti, Jijini Dar es Salaam.
Amesema Serikali inatambua mchango wa Taasisi za Dini katika kuimarisha mshikamano wa kijamii; kukuza maadili ya uadilifu, uwajibikaji na upendo; kutoa huduma za kijamii kama vile elimu, afya na msaada wa kijamii pamoja na kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa amani na mshikamano wa kitaifa.
“Serikali inatambua nafasi ya Jumuiya ya Waithna’ashariyyah Tanzania (TIC), ikiongozwa na Sheikh Mkuu wa TIC Maulana Sheikh Hemed Jalala na taasisi zote za dini katika kuimarisha mahusiano mema, amani na utuivu,” amesema.
Naye Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Waithna’ashariyyah Tanzania (TIC) Sheikh Hemed Jalala,ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa nia njema ya kushiriki katika Sherehe za Maulid, akisema ushiriki huo ni ishara ya ushirikiano mzuri kati ya Serikali na jamii.
Aidha, upendo na Huruma ndo Mafunzo ya Mtume Muhammad (S.W.W) ampapo amezitaka taasisi zote za dini kuendeleza juhudi za kuwaleta pamoja waumini na wasiokuwa waumini kupitia mihadhara na shughuli mbalimbali za kidini zinazolenga kumuenzi na kumsifia Mtume Muhammad (S.W.W), huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano na umoja katika jamii.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment