" DKT. NCHIMBI AFUKUZWA UANACHAMA CCM, NDEJEMBI KUCHUKUA NAFASI YAKE

DKT. NCHIMBI AFUKUZWA UANACHAMA CCM, NDEJEMBI KUCHUKUA NAFASI YAKE

Deogratius Ndejembi

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan 
imemvua uanachama aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, hatua iliyochukuliwa leo, siku moja baada ya kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa.

Uamuzi huo umefanywa na Halmashauri Kuu ya CCM katika kikao chake kilichofanyika leo, Agosti 26, 2026.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha Rose Migiro amesema “Kamati Kuu imejadili kuhusu suala la nidhamu na maadili ambalo lilikuwa linamkabili Emmanuel Nchimbi, na baada ya kuzingatia taarifa zote zilizokuwepo ilithibitika kwamba katiba ya CCM na kanuni zake zilikiukwa, na hivyo Nchimbi amefukuzwa uanachama”

Dkt. Nchimbi alitangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais na kustaafu shughuli za kisiasa jana, Agosti 25, 2026.

Katika hatua nyingine, Halmashauri Kuu ya CCM imepitisha jina la Deogratius Ndejembi kuwa mrithi wa Nchimbi katika nafasi hiyo.

Uamuzi huo unafungua ukurasa mpya katika uongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi, huku Ndejembi akitarajiwa kuchukua majukumu yaliyoachwa na Dkt. Nchimbi.

Mabadiliko hayo yamekuja katika kipindi ambacho CCM inaendelea kufanya maamuzi kuhusu muundo na uongozi wa chama pamoja na Serikali.

Post a Comment

Previous Post Next Post