Mkurugenzi
wa 'MAHONA CUP – 12', Patrick Mahona ametangaza kuongeza viwango vya zawadi kwa
timu zitakazoshiriki ligi hiyo na kuibuka mshindi wa 1 – 4.
Amefafanua
kuwa mshindi wa kwanza sasa atapata zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni
tano (5,000,000) pamoja na kombe, mshindi wa pili atapata fedha taslimu
shilingi milioni 2.5, mshindi wa tatu atapata shilingi laki tano na wa nne kusalia
na mipira miwili.
“Tumeboresha
viwango vya zawadi kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tatu, lkini mshindi wan ne
amebaki kwenye mipira. Nisisitize kwamba hapa bado sio mwisho, zawadi zinaweza
kubadilika na kuboreshwa zaidi wakati wowote.” Amesema Mahona ambaye pia ni
dwani wa kata ya Segese
Na
kuongeza “Kuna mdau ameguswa na ligi akaongeza dau, kwa hiyo tuendelee
kuifatilia ‘MAHONA CUP’ mambo mazuri yanakuja kwa vijana wetu, vipaji vipo, na
tunachotaka ni kuviibua sisi ngazi ya jamii ili ngazi za juu zione na
kuviendeleza.”
Hata
hiyo mkurugenzi huyo ameahidi pia kutoa zawadi kwa mchezaji bora, mfungaji bora
pamoja na kijana atakayeshiriki ligi akiwa na umri mdogo zaidi.
‘MAHONA
CUP’ imezinduliwa rasmi leo Agosti 26, 2026, katika viwanja vya shule ya msingi
Segese katika Halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama mkoani Shinyanga,
yakilenga kuibua na kuwasaidia vijana wenye ndota za kucheza soka kutimiza
ndoto zao.
Katika
mechi ya ufunguzi hii leo imekutanisha Itinde U20 Fc na uton Fc zote kutokea
kata ya segese ambapo Luton Fc imeibuka mshindi kwa kuichapa Itinde U20 goli 5
kwa 2, hivyo Itinde U20 inafungua dimba la kuyaaga mashindano haya muhimu kwa ukuaji
wa vipaji vya vijana.
HATUA YA MTOANO
Mechi ya ufunguzi Agosti 26, 2026 ni kati ya Itinde Fc na
Luton Fc, Agost 27, 2026 ni kati ya Supertiger Fc na Chemichemi Fc. Agost 28,
2026 ni kati ya Kilimanjaro Fc na Imani Academy, Agost 29, 2026 ni kati ya
Mlimani Fc na Newboys Ntobo. Agost 30, 2026 ni kati ya MAHONA Boys na Veterans
Fc.
Endelea
kutufuatilia…..

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254













Post a Comment