Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewatembelea wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Buhangija iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.Wakiadhimisha miaka ishirini ya Polisi Jamii mapema leo walianza na matembezi ya asubuhi yaliyoongozwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Janeth Magomi ili kuhamasisha Amani, Usalama na Umoja kwa Kitaifa kama isemavyo kauli mbiu ya miaka ishirini ya Polisi Jamii Baada ya matembezi hayo walipata wasaa wa kuwatembelea watoto wenye mahitaji maalum kwa lengo la kupata nao chakula cha mchana na kuwapatia mahitaji mbalimbali iwasaidie kusoma bila changamoto.Kwa upande wake mkuu wa Polisi Jamii katika Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Fraterine Tesha alitoa nafasi ya elimu ya ukatili kutolewa shuleni hapo ili kusaidia watoto hao kuondokana na changamoto hiyo ya ukatili ambapo Mkuu wa Dawati la Jinsia Wilaya ya Shinyanga Mkaguzi wa Polisi Jane Mwazembe alitoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi hao na kuwaeleza namna ya kuepuka vitendo hivyo na maeneo ya kuyatolea taarifa.Aidha Mwl Edward Mdagata akimuwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga alitoa shukrani zake kwa Jeshi la Polisi kwa kuona haja ya kuwatembelea wanafunzi hao na kusema kuwa kufanya hivyo ni kujenga jamii ya watoto watakaoshirikiana na Jeshi la Polisi bila woga kwani nao wataona Polisi ni sehemu ya jamii na watatoa ushirikiano wao kikamilifu kwa Jeshi la Polisi katika kupinga ukatili na uhalifu.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment