SERIKALI imechukua hatua kulinda na kuendeleza rasilimali za kiakili nchini kutokana na uzinduzi rasmi wa Programu ya InnoIP Tanzania, mkakati mahususi unaolenga kuwaongoza wabunifu, watafiti na kampuni changa kulinda, kusimamia na kuifanya ubunifu kuwa biashara kutoka hatua ya wazo hadi kufika sokoni.
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH kwa kushirikiana na Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni BRELA imezindua rasmi Programu ya InnoIP Tanzania yenye lengo la kuwasaidia wabunifu kutokawazo hadi fursa za miliki bunifu, kulinda ubunifu, kujenga thamani na kuharakisha biashara.
Uzinduzi huo ulifanyika mkoani Tanga ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batilda Buriani ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Dk Batilda alisema kuwa nchi inahitaji kuzalisha maarifa na teknolojia mpya, huku ikihakikisha kazi hizo zinalindwa kisheria ili kuleta tija ya kiuchumi na kijamii, ingawa tathmini inaonesha kuwa wabunifu wengi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ikiwemo kuweka wazi mawazo yao mapema bila makubaliano ya umiliki, kutoweka kumbukumbu sahihi na kuchelewa kushughulikia masuala ya miliki ubunifu hadi bidhaa ziingie sokoni.
Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Amos Nungu alisema hatua hiyo inadhihirisha dhamira ya serikali katika kubadili mawazo ya Watanzania kuwa bidhaa na huduma zenye tija kiuchumi, akieleza kuwa mpangilio huo unatoa mwongozo na msaada wa vitendo kwa wabunifu ili kubadilisha mawazo yao kuwa bidhaa halisi zinazoweza kuuzwa sokoni.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Godfrey Nyaisa alisema mradi huo utasaidia usajili na ulinzi wa kazi za wabunifu kupitia ushirikiano wa karibu na Brela ili kuzuia wizi wa ubunifu, ukimhusisha pia mdau mkubwa kama vile Airtel Tanzania, watafiti, vyuo vikuu, vituo vya atamizi, wawekezaji na wajasiriamali hasa wanawake kupitia programu ya Fursa Women.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment