" SHINYANGA KUPOKEA MWENGE WA UHURU

SHINYANGA KUPOKEA MWENGE WA UHURU

Mbio za Mwenge wa Uhuru zinatarajiwa kuwasili Mkoani Shinyanga Agosti 19, 2026, ukitokea Mkoani Mwanza na kupokelewa katika Kata ya Kolandoto, huku ukitarajiwa kukimbizwa jumla ya kilomita 84.8 ndani ya Manispaa ya Shinyanga.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze amesema Mwenge huo utatumika kufikia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya kuzinduliwa, kuwekwa mawe ya msingi, kufunguliwa na kukaguliwa, pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.

Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji Kolandoto, ambao utazinduliwa mara baada ya mapokezi ya Mwenge, pamoja na shughuli katika Zahanati ya Mwasalele zinazohusisha huduma za afya na elimu kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Mwenge pia utafika Makindo Royal Hotel, ambako kutawekwa jiwe la msingi la mradi wa uwekezaji wa sekta binafsi, kabla ya kuelekea katika eneo la mradi wa nishati kwa ajili ya uzinduzi na uhamasishaji kuhusu matumizi sahihi ya nishati.

Aidha, Mwenge utafikia Daraja la Dodoma, ambako kutafanyika ufunguzi wa daraja hilo, hatua inayolenga kuboresha usafiri na mawasiliano kwa wananchi.

Katika sekta ya elimu, Mwenge utafika Shule ya Sekondari Rajani na Shule ya Sekondari Old Shinyanga, ambako pamoja na shughuli za ujumbe wa Mwenge, wananchi watahamasishwa kuhusu umuhimu wa elimu na ushiriki wa jamii katika kuboresha mazingira ya kujifunzia.

Mkurugenzi huyo amesema pia Mwenge utafika Kata ya Kambarage, katika eneo la Mkesha wa Mwenge wa Uhuru Kitaita, ambako utakagua na kuzindua shughuli za vijana pamoja na mabanda yanayotoa elimu kuhusu dawa za kulevya, uchangiaji wa damu salama, lishe, rushwa na VVU/UKIMWI.

Aidha, vikundi vya vijana na shughuli zao za kiuchumi vitakaguliwa kwa lengo la kuhamasisha vijana kutumia fursa za kujiajiri na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii.

Kwa ujumla, Mkurugenzi amesema ziara hiyo inalenga kuhamasisha wananchi kuhusu maendeleo, afya, elimu, maji, nishati, miundombinu, uwekezaji, uwezeshaji wa vijana na uwajibikaji, huku wananchi wakihimizwa kushiriki katika kusimamia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukabidhiwa kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Agosti 20, 2026, katika Shule ya Msingi Tinde A, baada ya kukamilisha safari yake ya kilomita 84.8.

 

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post