Na Tonny Alphonce -Misalaba Mwanza
Shirika la Posta Tanzania limeboresha huduma ya EMS, hatua inayolenga kuwawezesha wananchi na wafanyabiashara kusafirisha nyaraka, vifurushi na mizigo kwa haraka, usalama na urahisi zaidi.
Meneja Mauzo wa Shirika la Posta Tanzania, Philip Kowero, amesema maboresho hayo yanaenda sambamba na uwekezaji mkubwa katika teknolojia ya kidijitali, unaolenga kuwawezesha wananchi kupata huduma bila kulazimika kufika katika ofisi za Posta.
“Hivi sasa unaweza kudownload app ya Posta Kiganjani na kupata huduma zote bila kufika ofisi za Posta,” amesema Kowero.
Kwa upande wake, Meneja wa EMS, Ahamad Rashid, amesema maboresho ya huduma hiyo yatawasaidia wananchi kupata huduma za usafirishaji kwa haraka na kwa usalama.
Ameutaka umma kutumia huduma ya EMS bila wasiwasi, akisisitiza kuwa Shirika la Posta ni taasisi iliyo chini ya Serikali.
📦 EMS – Usafirishaji wa haraka na salama.
#ShirikaLaPosta #EMS #PostaTanzania #PostaKiganjani #Usafirishaji #Biashara #HudumaKwaWananchi #DigitalTanzania #Tanzania
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment