Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Marco G. Chilya, amewataka Maafisa, Wakaguzi, Askari wa vyeo mbalimbali pamoja na Wananchi kutumia michezo kama jukwaa muhimu la kudumisha amani, upendo, mshikamano na kujenga mahusiano mazuri kati ya Jeshi la Polisi na jamii.
Wito huo umetolewa Agosti 25, 2026 katika Uwanja wa Majimaji, Manispaa ya Songea, wakati wa Bonanza la Polisi Jamii Cup, lililoandaliwa kuelekea maadhimisho ya Miaka 20 ya Polisi Jamii huku Bonanza hilo likihusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, riadha za mita 100 na 200 kwa wanawake na wanaume pamoja na mchezo wa kuvuta kamba, ambapo Polisi walishindana na timu kutoka katika jamii.
Katika mchezo wa mpira wa miguu kati ya timu za Shule za Sekondari Songea Boys na Emmanuel Nchimbi, timu ya Emmanuel Nchimbi iliibuka mshindi kwa bao 1-0 huku mashindano hayo yakiendelea kwa kuwashirikisha wananchi na askari katika michezo mbalimbali, hatua iliyolenga kuimarisha uhusiano, ushirikiano na kupeana elimu kuhusu umuhimu wa kushirikiana katika kudhibiti uhalifu katika jamii.
Katika fainali ya mpira wa miguu, timu ya Polisi Wilaya ya Nyasa ilikutana na timu ya FFU Ruvuma, ambapo FFU Ruvuma iliibuka mshindi kwa mikwaju ya penalti na kutwaa Kombe la mashindano hayo.
Washindi katika michezo mbalimbali walikabidhiwa zawadi ikiwemo medali, mipira na Kombe, ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi na ushiriki wao katika kufanikisha bonanza hilo.
Akiongea Kamanda Chilya SACP, amesisitiza kuwa michezo si kwa ajili ya burudani pekee, bali ni nyenzo muhimu ya kuwakutanisha watu, kujenga urafiki, kuimarisha mshikamano na kutoa fursa ya kuelimishana kuhusu madhara ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu huku akiongeza kuwa ushirikiano kati ya Polisi na wananchi ni msingi muhimu katika kuzuia na kudhibiti uhalifu pamoja na kujenga jamii salama na yenye amani.
Aidha, SACP Chilya amewapongeza Maafisa, Wakaguzi, Askari wa vyeo mbalimbali pamoja na wananchi wote walioshiriki katika Bonanza hilo na kuwataka kuendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kupitia michezo na shughuli nyingine za kijamii huku akisema michezo ya mara kwa mara itaendelea kuwa chachu ya kuimarisha amani, upendo, mshikamano na ushirikiano, hivyo kuongeza ufanisi katika mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu na wahalifu katika jamii.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment