
Watendaji wa Serikali kuanzia ngazi za mtaa hadi wilaya wametakiwa kushughulika na kutatua shida na changamoto za wananchi katika maeneo yao.
Wito huo umetolewa leo hii na Mkuu wa wilaya ya Ilala Mheshimiwa Edward Mpogolo wakati wa zoezi la upandaji miti na usafi wa mazingira katika kata za Chanika na Zingiziwa.
Mhe. Mpogolo amesema viongozi hao wameaminiwa na Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa leongo la kumsaidia katika maeneo yao hivyo hawana budi kuhakikisha wanazichukua changamoto za wananchi kama zao.
"Mheshimiwa Rais anajitahidi sana kuleta fedha za miradi ya maendeleo katika maeneo yetu, yeye hawezi kuja kutatua shida ndogondogo za watu, shida hizi ni zetu sisi". Alisema
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha na kuwataka viongozi wa Halmshauri hiyo kuendelea kusimamia uadilifu.
Zoezi hilo la upandaji miti lililoongozwa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe. Bakari Shingo limefanyika Zahanati ya Nzasa kata ya Zingiziwa likihusisha wadau mbalimbali wa Mazingia wakiwemo Chama cha Skauti Tanzania.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment