" UBUNIFU UNATAKIWA KUTUMIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZA SEKTA YA BAHARI – PROF. GURUMO

UBUNIFU UNATAKIWA KUTUMIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZA SEKTA YA BAHARI – PROF. GURUMO

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Prof. Tumaini Gurumo, amesema ubunifu una nafasi kubwa katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya Bahari pamoja na sekta nyingine katika jamii. Prof. Gurumo amesema hayo Agosti 17, 2026, Jijini Tanga katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu.

Amesema DMI imeshiriki maonesho hayo kwa lengo la kuonesha bunifu mbalimbali zilizofanywa na wanafunzi pamoja na taasisi hiyo katika kipindi cha hivi karibuni, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika elimu, ujuzi na ubunifu. Prof. Gurumo amesema ubunifu unaofanywa na wanafunzi na wataalamu wa DMI unalenga kutoa majibu kwa changamoto mbalimbali kwenye jamii, hususan katika sekta ya Bahari, ambayo ni muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

Aidha, amesema chuo hicho kinatarajia kufanya Kongamano la Tano la Uchumi wa Bluu Jijini Dar es Salaam, kuanzia Septemba 7 hadi 9 mwaka huu litakalowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya Bahari kutoka ndani na nje ya nchi kujadili fursa, changamoto na mikakati ya kuendeleza sekta hiyo, huku akisisitiza kuwa kila mmoja ni mdau wa sekta ya Bahari na ananufaika kwa namna moja au nyingine na shughuli zinazohusiana na Bahari.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post