Ujenzi wa jengo jipya la maonesho la Halmashauri ya Mji Kasulu unaoendelea katika Viwanja vya Ipuli, Manispaa ya Tabora umefikia zaidi ya asilimia 70 ambapo mradi huo unalenga kuboresha mazingira ya ushiriki wa Halmashauri katika Maonesho ya Nanenane na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi na wadau.Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Julius Simbeye amesema kukamilika kwa jengo hilo kutachangia kuongeza idadi ya wakulima na wadau watakaoshiriki maonesho hayo kila mwaka.Ameongeza kuwa jengo hilo litakuwa chachu kwa wajasiriamali kuonesha teknolojia na bidhaa mbalimbali watakazokuwa wanazalisha hatua itakayoongeza ufanisi katika uzalishaji na kuongeza masoko.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254







Post a Comment