" WAKARIBISHWA KUJIFUNZA KILIMO CHA MKATABA KWA MAZAO YA MAHINDI NA ALIZETI

WAKARIBISHWA KUJIFUNZA KILIMO CHA MKATABA KWA MAZAO YA MAHINDI NA ALIZETI



KAMPUNI ya Kazimiry Enterprise Company Limited Imezamilia kuwaelimisha watu juu ya kilimo cha zao la Alizeti na Mahindi kwa njia ya mkataba kuwezesha kupatikana kwa mafanikio kwenye sekta ya kilimo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Kazimiry Ltd, Silas Kazimiry  alisema leo jijini Mwanza kuwa ulimaji wa zao hilo kwa njia ya mfumo wa kilimo cha mkataba ni mkombozi kwa wakulima wengi hapa nchini.

Lengo la kuwakutanisha wadau wa kilimo ni kujifunza namna ya kutumia fursa za kilimo cha mkataba kufikia malengo ya kujikomboa kiuchumi kupitia fursa zinazopatikana  kutokana na mazao.

Alisema kuwa watawafundisha namna  ya uchakataji  wa mazao kwenye viwanda vyao saba vilivyo katika eneo moja kutengeneza bidhaa aina ya Boneka kwa kutumia   mahindi na alizeti.

Bidhaa hizo za Boneka zitachakatwa kwa kutengenezwa premium sunflower oil, Boneka Sembe, Boneka mchele, Boneka ethanol na Boneka charcoal briqquttes.


Utengenezaji wa bidhaa hizo utawafanya kuwa na ufundi wa kujiajiri wenyewe kwa kuchakata mazao hivyo kuyaongezea thamani kwa kutumia alizeti na mahindi hivyo kuwafanya waweze kuwa na namna kujiingizia kipato.

Post a Comment

Previous Post Next Post