" WAKATOLIKI WASEMA WALICHOZUNGUMZA NA SAMIA

WAKATOLIKI WASEMA WALICHOZUNGUMZA NA SAMIA

 


Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limesema mkutano wao wa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan uliombwa nao kwa lengo kuu la kumkabidhi andiko maalum linaloeleza mtazamo wao kuhusu hali ya kisiasa nchini .
Pia wanasema waraka waliokabidhi umelenga pia kuzungumzia uimarishaji wa mazungumzo ya kitaifa yanayolenga kujenga amani, ukweli, msamaha na uponyaji wa taifa.

Katibu Mkuu wa TEC, Padri Dk Charles Kitima, alisema hayo kupitia picha jongefu iliyosambazwa kwa umma kuhusu mazungumzo yaliyofanyika kati ya maaskofu na Rais Samia jijini Dodoma, Agosti 10, 2026.

Alieleza kuwa hatua hiyo ya kutaka kumuona Rais Samia ilitokana na azimio la kikao cha mwaka cha maaskofu kilichofanyika mwezi Juni, ambapo viongozi hao waliona umuhimu wa kuendelea na mazungumzo yaliyoanza mwaka uliopita ili kutimiza wajibu wao wa kimaadili wa kuelimisha jamii kuhusu utu, upendo, na kuishi kindugu.

Kupitia mazungumzo hayo, maaskofu walisisitiza kuwa mazungumzo na kukiri ukweli ni njia muhimu ya kuvuka migogoro kama inavyoshuhudiwa katika nchi nyingine duniani, huku wakikumbusha wajibu wa viongozi wa dini katika kuhamasisha amani na kuheshimu utu wa binadamu chini ya mamlaka ya maamuzi na utekelezaji iliyo mikononi mwa serikali.

Aidha, TEC imeahidi kuendelea kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali ili kuhakikisha utulivu na mshikamano wa Watanzania unadumishwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post