Meneja wa tawi Benki ya Azania, Ambokile Tuntufye akimkabithi zawadi Mkuu wa wilaya ya Hai mara baada ya kutembelea banda hilo Nanenane ,Njiro .

Happy Lazaro,Arusha

Arusha .BENKI ya Azania imewahimiza wakulima, wafanyabiashara wa mazao na wauzaji wa bidhaa nje ya nchi kutumia huduma mbalimbali za kifedha zinazotolewa na benki hiyo ili kuongeza uzalishaji na kupanua masoko ya biashara zao.

Benki hiyo imeeleza kuwa inatoa huduma ambazo huwasaidia wafanyabiashara kufanya miamala ya kimataifa kwa usalama na uhakika wa malipo.

Akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Hai mara baada ya kutembelea banda hilo katika maonesho ya nanenane,Meneja wa tawi Benki ya Azania, Ambokile Tuntufye amesema kuwa ,benki hiyo inatoa mikopo yenye riba nafuu kwa wafanyabiashara wa mazao ili kuwawezesha kununua mazao kutoka kwa wakulima, kuyahifadhi na kuyauza kabla ya kurejesha mikopo hiyo.

Tuntufye amesema kuwa ,Benki hiyo ina huduma za kifedha zinazowafaa watu wa makundi yote, kuanzia akaunti za watoto wachanga hadi huduma kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, sambamba na bidhaa nyingine mbalimbali za benki.

Tuntufye ameongeza kuwa, ushiriki wa wananchi katika maonesho ya mwaka huu umeongezeka kwa kiwango kikubwa, jambo lililowapa fursa ya kuwafikia wateja wengi na kuwapatia elimu kuhusu huduma wanazotoa.

Ameongeza kuwa ,benki hiyo itaendelea kushiriki katika maonesho hayo na kuwakaribisha wananchi kutembelea banda lao ili kupata ushauri na kufahamu bidhaa mbalimbali za kifedha zinazoweza kuwasaidia kukuza shughuli zao za kilimo na biashara.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Hai ,Hassan Bomboko akizungumza mara baada ya kutembelea banda hilo la Azania benki katika maonesho ya Nanenane, ameipongeza benki hiyo kwa kuendelea kuwa miongoni mwa taasisi za kifedha zinazochangia maendeleo ya wananchi kupitia huduma zinazowagusa moja kwa moja wakulima, wafugaji na wafanyabiashara.

Bomboko amesema kuwa,ameridhishwa na huduma na taarifa alizopewa katika banda hilo, akieleza kuwa zinaonyesha mwelekeo sahihi wa kuiwezesha sekta ya kilimo kupitia huduma za kifedha zinazowafikia wakulima wa ngazi zote, kuanzia wadogo, wa kati hadi wakubwa.

Pia ameitaka benki Azania kuendelea kupanua wigo wa huduma zake ili kuwafikia wananchi wengi zaidi, hususan katika Kanda ya Kaskazini na Mkoa wa Kilimanjaro, ikiwemo Wilaya ya Hai, ambako kuna idadi kubwa ya wakulima, wafugaji na wafanyabiashara wanaohitaji huduma za kifedha.

Ameongeza kuwa, akiwa pia ni mkulima, amejifunza mambo mbalimbali kupitia maelezo aliyopatiwa na ameahidi kuwa balozi mzuri wa benki hiyo kwa kuwahamasisha wananchi wengine kutumia huduma zake ili kukuza shughuli zao za uzalishaji na biashara.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254