Watu 12 wakiwemo askari polisi watano na mahabusu saba wamefariki dunia katika ajali mbaya iliyotokea leo katika eneo la Mlima Sekenke, Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Ajali bhiyo ilihusisha gari la Jeshi la Polisi na lori la mizigo lililokuwa limefeli breki.
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa moja na dakika 30 asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Nzega, eneo la Kijiji cha Misigiri, Kata ya Ulemo, wakati gari hilo la polisi lilipokuwa likisafirisha mahabusu kutoka Kituo cha Polisi Shelui kuelekea Mahakama ya Wilaya ya Iramba iliyopo Kiomboi.
Lori lililohusika ni lenye namba za usajili RAF 243X/TRL 4255 mali ya kampuni ya YYUSSA ya Kigali, Rwanda, lililokuwa likisafirisha mafuta ya dizeli kutoka Bandari ya Dar es Salaam kuelekea Rwanda.


Imeelezwa kuwa, likiwa linashuka mlima huo breki zilifeli na kuligonga gari la Polisi aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili PT 1982.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa taarifa zaidi zitatolewa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Kufuatia msiba huo , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus Wambura, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Omary Dendego, familia za marehemu, ndugu, jamaa na Watanzania wote, huku akiwakumbusha madereva wote nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuhakikisha vyombo vya moto viko salama kabla ya safari ili kulinda maisha ya wananchi.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment