" AOMBA MSAADA KUMTIBU MWANAYE

AOMBA MSAADA KUMTIBU MWANAYE



MAMA Joyce Waryoba wa Nyamhongolo Jijini Mwanza mwenye mtoto aliye na ugonjwa wa degedege na mifupa legelege anaomba jamii ya watanzania wamsaidie kumchangia pesa kwa ajili ya kumtibu mtoto wake.

Mwanaye Elizabeth Juma mwenye umri wa miaka (14) amekuwa na tatizo hilo linalomfanya asiweze kutembea wala kufanya kitu chochote hivyo kumfanya mama yake amuhudumie kwa kila kitu.

Mama mzazi wa mtoto huyo anasema tangia mwanaye azaliwe amekuwa akisumbuliwa na maradhi hayo hali inayomfanya kushindwa kujishughulisha na kazi zingine. 



Anasema mtoto huyo anatakiwa kula chakula kilaini kwani meno yake ni mabovu hawezi kula chakula ambacho si laini.

Mama huyo anaomba kwa watu wote waweze kuguswa na wito huo hivyo waweze kumsaidia ili aweze kumpeleka mwanaye katika hospitali ya Bugando.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652


Post a Comment

Previous Post Next Post