" BARABARA LUMUMBA ‘B’ MTAA WA IGALILIMI MLIMANI YAFUNGUKA, IGALILIMI KUWA KITOVU CHA BIASHARA KAHAMA

BARABARA LUMUMBA ‘B’ MTAA WA IGALILIMI MLIMANI YAFUNGUKA, IGALILIMI KUWA KITOVU CHA BIASHARA KAHAMA

 

Barabara ya lumumba B iliyopo mtaa wa igalilimi Mlimani, Kata ya Kahama Mjini, Manispaa ya Kahama, imeanza kuleta unafuu kwa watumiaji baada ya kufunguliwa na kufanyiwa maboresho. Maboresho hayo yanafanyika kupitia fedha zilizotenga na Manispaa kupitia baraza la madiwani zaidi ya Shilingi milioni 300 kwa ajili ya kata 20 za manispaa hiyo kwa lengo la ukarabati wa barabara korofi. Diwani wa kata yaKahama Mjini, Godson Andrew, amesema barabara hiyo yenye urefu wa takribani kilomita moja, ilikuwa haipitiki kwa urahisi, lakini juhudi zilizofanyika katika kipindi cha miezi miwili zimeanza kurahisisha matumizi ya barabara hiyo. “Ni barabara ya siku nyingi ambayo ilikuwa bado haijawahi kufanyiwa marekebisho, Ilikuwa haipiti magari. Hata bodaboda zilikuwa zinapita kwa shida kwa sababu ya mawe makubwa yaliyokuwepo.” Amesema Andrew Amesema kukamilika kwa barabara hiyo kunaweza kuifungua zaidi igalilimi kiiashara, kutokana na eneo hilo kuwa karibu na maeneo yenye mkusanyiko wa watu na shule. Amesema changamoto kubwa iliyopo katika uboreshaji wa barabara hiyo ni mawe makubwa yanayohitaji nguvu kazi kubwa kuyaondoa, huku kazi ikiendelea hatua kwa hatua kwa kutumia rasilimali zilizopo. Mwendesha pikipiki Matayo Elia amesema kufunguliwa kwa barabara hiyo tayari kumeleta mabadiliko katika shughuli zake za kila siku. “barabara ikitengenezwa ikafunguka, itatusaidia kwa sasa hivi ikitengenezwa ikafunguka, tutapita kwa urahisi na airia wetu, na hata kwa watembea kwa miguu watauwa wamerahisishiwa.” Barabara hiyo inaanzia nyuma ya kituo kikuu cha polisi Kahama, na kuelekea upande wa kanisa laMoravian nyihogo.

Post a Comment

Previous Post Next Post