Zaidi ya vijana 1,300 wameshiriki Kongamano la Vijana 2026 la Halmashauri ya Mji Kasulu lenye lengo la kuwaunganisha vijana kujadili masuala ya uraia, fursa za kiuchumi, changamoto mbalimbali wanazokutana nazo na njia bora ya kuzitatua kwa faida na manufaa yao na Taifa kwa ujumla.Kongamano hilo limefanyika Septemba 05, 2026 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kasulu (Kasulu TTC) na kuwakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.Akifungua kongamano hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaac Anthony Mwakisu amewataka vijana kujishughulisha, kuwa wazalendo, kulinda amani na kutumia vyema fursa zilizopo katika kujenga maisha yao na kuunga mkono juhudi zote za Serikali katika kuchochea maendeleao.Aidha, Kanali Mwakisu amewahimiza vijana kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru unaotarajia kuwasili Halmashauri ya Mji Kasulu Septemba 10, 2026. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia Julius Simbeye amewataka vijana kuendelea kuuunga mkono juhudi za Serikali, kuketi na kujadili namna ya kupata suluhisho la changamoto zinazowakabili kwa kushiriki makongamano na vikao vinavyowahusu.Naye Amina Kaniki, mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, amewahimiza vijana kutumia teknolojia kwa tija ili kujenga uchumi wao na kunufaika na fursa mbalimbali zinazopatikana.Kongamano hilo limejikita kujadili mada mbalimbali zikiwemo Uraia, Uzalendo, Amani, Uwajibikaji, Uadilifu, fursa za kiuchumi, mikopo, mitaji, biashara na fursa za uwezeshaji kwa vijana.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254














Post a Comment