Na Mapuli Kitina Misalaba
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
limewajengea uwezo waandishi wa habari mkoani Shinyanga kuhusu sekta ya mafuta
na gesi asilia pamoja na miradi ya kimkakati, ikiwemo Bomba la Mafuta Ghafi la
Afrika Mashariki (EACOP).
Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo, Septemba 4,
2026, katika Ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga, yakilenga kuongeza uelewa
wa waandishi kuhusu shughuli za TPDC, fursa zinazotokana na miradi hiyo pamoja
na wajibu wa jamii katika kulinda miundombinu ya Taifa.
Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Shinyanga, David Lyamong’i, amesema waandishi wa habari wana wajibu wa kutoa
taarifa sahihi kuhusu miradi ya mafuta na gesi, kueleza manufaa yake kwa
wananchi na kuhamasisha jamii kulinda miundombinu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na
Mawasiliano TPDC, Marie Msellemu, amesema warsha hiyo ni sehemu ya mkakati wa
shirika kuwa karibu na wadau wake na kuwawezesha waandishi kuelewa sekta ya
mafuta na gesi pamoja na fursa zinazotokana na miradi hiyo.
Akizungumzia EACOP, Kaimu Mratibu wa Mradi huo kwa
upande wa TPDC, Jumanne Mohamed, amesema matarajio ni kwamba ifikapo Januari
15, 2027, mafuta yataanza kuingizwa kwenye bomba na kusafirishwa kuelekea
Chongoleani mkoani Tanga.
Amesema katika Wilaya ya Kahama, mradi huo umepita
katika vijiji na mitaa 16, huku kaya 10 zilizoathiriwa na utekelezaji wa mradi
huo zikilipwa fidia yenye thamani ya takribani Shilingi bilioni 1.8.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa
Shinyanga, Greyson Kakuru, ameishukuru TPDC kwa mafunzo hayo, akisema
yamewaongezea waandishi ujuzi wa kuandika kwa ufasaha na kutoa taarifa sahihi
kuhusu masuala ya mafuta, gesi asilia na miradi ya kimkakati.
Katika mafunzo hayo, TPDC pia imeeleza kuhusu shughuli
za utafutaji wa mafuta na gesi zinazoendelea katika Bonde la Eyasi-Wembere,
linalohusisha maeneo ya Mkoa wa Shinyanga, ikiwemo Wilaya ya Kishapu.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026. Kaimu Mratibu wa Mradi wa EACOP-TPDC, Jumanne Mohamed, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka TPDC, Jenifa Mshanga, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na TPDC.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi, maafisa wa TPDC pamoja na waandishi wa habari walioshiriki mafunzo kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi, maafisa wa TPDC pamoja na waandishi wa habari walioshiriki mafunzo kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na TPDC

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Mkurugenzi wa Misalaba Media, Mapuli Misalaba, akishiriki kwenye mafunzo hayo.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Kaimu Mratibu wa Mradi wa EACOP-TPDC, Jumanne Mohamed, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.

Post a Comment