Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ameliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria msanii Godfrey Tumaini maarufu Dudubaya, baada ya kushindwa kuitikia wito wa Wizara hiyo.
Katambi amesema Dudubaya alikuwa ametakiwa kufika Wizara ya Mambo ya Ndani baada ya kutajwa katika tuhuma za makosa ya jinai, lakini licha ya kuitwa kwa mara ya pili, bado hakufika.
Waziri amesema Dudubaya ameonekana kwenye mitandao ya kijamii akitoa kauli ambayo Waziri ameielezea kuwa ni
kukaidi wito wa Serikali.
Kutokana na hali hiyo, Katambi ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha Dudubaya anapatikana kokote aliko na kufikishwa mbele ya Jeshi hilo ili achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

Post a Comment